Waka Flocka amchagua Karruaeche dhidi ya Rihanna, asema hajavutiwa kuwa kwa Rihanna.



Rapper kutoka Atlanta Wacka Flocka hivi karibuni ameelezea mtazamo wake kuhusu ile quarrel inayowahusisha warembo wawili Karruache Tran na the R&B diva Rihanna ambao ex-boyfriend wao Chris Breezy alisema anawapenda wote.
Waka Flocka yeye amesema kama angepewa nafasi ya kuchagua yupi wa kumuunga mkono katika mtafaruku huo asingemchagua Rihanna kabisa, kwa hiyo hii inamaanisha anamsupport Karruache Tran.
“Mi niko katika mahusiano,” alianza kusema Wacka Flocka katika interview. Akaendelea “nilikuwa na mpenzi kwa miaka kama miwili hivi. Alikuwa anaelekea kuwa na maisha kama hayo. …mimi nauhakika kabisa nisingekuwa upande wa Rihanna, sio kama nasema Rihanna ni mbaya, siyo hivyo. She’s got history. Unajua ninachomaanisha?” alisema Waka Flocka.
lakini inaonekana alijua kabisa hii inaweza kuleta mkanganyiko hivyo akasisitiza kuwa huu ni mtazamo wake kama angepewa nafasi ya kuchagua nani anaemsupport kati ya hawa warembo wawili katika hii issue ya Chris Breezy. “ Simhukumu mtu yeyote hapa, unajua huwezi kujua nini hasa kiko kati yao, they’re in their beds. kwa hiyo huwezi kujua kiundani nini kinaendelea kati yao.”
Haya ndiyo mawazo ya rapper huyo toka Atlanta kuhusu kile ambacho kilihit mitandao mbali mbali wiki iliyopita ambapo Chris Breezy alitangaza kumuacha Karruache T eti ili asiharibu urafiki wake na Rihanna na asiendelee kumuumiza, lakini baadae akakiri kupitia video clip kuwa anawapenda wote wawili Rihanna na Karruache Tran.

No comments:

Post a Comment