Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.


Mikasa yamuandama Justine Bieber,Baada ya kuibiwa laptop kwenye show, sasa adondoka kwenye ngazi wakati anaperform.

Mikasa inazidi kuiandama tour ya ‘Believe’ ya Justine Bieber ikiwa ni siku chache baada ya kuibiwa laptop yake akiwa stejini huko Arizona Washington, sasa amepata mkasa mwingine baada ya kuanguka alipokuwa anaperform huko Saskatchewan Canada usiku wa October 17.

Bieber alikuwa anakaribia mwishoni kabisa kumalizia wimbo wake wa Beautiful aliokuwa anaupiga na Carly Rae Jepsen, msichana huyo alishuka kwenye ngazi za steji akiwa na Justine Bieber, lakini kwa bahati mbaya Bieber alimiss step moja kwenye ngazi akakosa balance na akaanguka.
Baada ya tukio hilo immediately Jepsen alimshika mkono Bieber na kumuinua, na mkali huyo aliweza kusimama na kuendelea kumalizia perfomance yake kama vile hakuna kitu kam hicho kilichotokea pale.
Mkali huyo ambae ni boyfriend wa Selena Gomez anatarajia kuendelea na tour yake ‘Believe’ hadi mwakani. na ratiba yake inaonesha kuwa baada ya hiyo show ya Saskatchewan ataelekea Winnepeg na Minneapolis kati ya October 18-20. na baada ya hapo anatarahji kuingia Ulaya around February 2013.

No comments:

Post a Comment