Game amkingia kifua muigizaji Stacey Dash “Sio kila mtu mweusi anamsapoti Obama”


Stacey Dash

Rapper Game ambae hivi karibuni alisema kuwa anamsapoti Barack Obama no matter what, ameamua kumtetea muigizaji wa kike Stacey Dash baada ya msichana huyo kusema kuwa yeye atampigia kura Mitt Romney japokuwa ni mtu mweusi na hivyo watu wengi kuonekana wanamshangaa sana na kumsakama muigizaji huyo wa kike kwa uamuzi wake huo.
Member huyo wa zamani wa G-Unit amesema anaheshimu sana itikadi ya kisiasa ya mrembo huyo anaefanya vizuri kwenye tasnia ya uigizaji, Game alifunguka, “nashindwa kuelewa tatizo la watu katika hili, tunaishi katika dunia ambayo tunajaribu kama watu kuondokana na ubaguzi wa rangi. Sio kila mtu mweusi duniani anamsapoti Obama…why are we slamming her?” Game aliendelea, “labda ana mtazamo tofauti na maoni tofauti, na inabidi afungamane nayo.”
Dash hivi karibuni alielezea vikwazo alivyo na mitazamo hasi aliyopokea baada ya kuweka wazi mtazamo wake kuwa atampigia kura Romney.

No comments:

Post a Comment