Connection kati ya Obama na wanawake yainasa kura ya Alicia Keys “Obviously I’m an Obama Supporter”



Wakati joto la uchaguzi wa urais wa Marekani linazidi kupanda kila sekunde na kila celeb kutoa maoni yake kwa yule anaemsupport kati ya Romney na Obama, No one hit maker Alicia Keys ameamua kuiweka hadharani kura yake baada ya kupima na kuona kuwa inafaa kumsuport yule ambae anaona atafaidika nae akiwa rais wa United States.
Alicia keys ameweka wazi kuwa anamsuport Barack Obama na kwa hali hiyo ndiye atakae mpigia kura yake. Pamoja na sababu nyingine alizozitoa lakini swala la kuwawezesha wanawake na kuwaheshimu lilichukuwa asilimia nyingi sana, na kuongezea na connection kati ya Obama na umuhimu wa wanawake.
Alicia Keys alifunguka kiivo baada ya kumaliza tu kuongea katika women’s Vote Summit huko Philadelphia ambapo alipiga story na mtandao wa SOHH kuhusu umuhimu wa wanawake kuhakikisha sauti zao zinasikika katika uchaguzi wa uraisi wa Marekani mwezi ujao.
Pamoja na kuweka wazi kura yake bado Alicia aliwaambia wanawake wampigie kura yule wanajisikia ni bora zaidi kati ya wagombea hao wa Uraisi wa Marekani.

 “Nadhani sisi kama wanawake tunaulazima wa kuitumia vizuri sauti yetu kusimama kwa ajili ya mtu ambae atatupa heshima tunayositahili kama wanawake katika nchi hii. Tumepiga hatua kubwa sana kwa miaka mingi na hakuna sababu ya kurudi nyuma tena.” Alisema Alicia na kuongeza kuwa “obviously I’m an Obama Supporter.”
Alipoulizwa sababu zinazomfanya ampe nafasi hii Barack Obama, alisema “he has been raised by a strong super woman; he married a super strong woman; he’s raising two credibly strong women; so he is personally connected to what is important with women’s issues.”
The R&B queen alimaliza kwa kusema anadhani hicho ni kitu kikubwa sana na hawawezi kukiacha kiende hivi hivi. Keys alisisitiza “tunatakiwa kuwa really, really, really focused katika kuhakikisha kila mwanamke anaenda kumpigia kura mtu ambae tunajua atakuja kuendeleza kutu-encourage sisi na kupata kila kitu ambacho tunastahili. Chochote kinyume na hapo kitakuwa sio sahihi.” Alimaliza Alicia Keys.
Inaonekana Obama upepo wake kwa celebs ni mzuri sana na kama tunavyojua hawa wana ushawishi mkubwa sana kwa watu. Hivi karibuni Snoop Lion aliweka wazi kuwa anamsuport Obama, Nick Minaj nae alishtua kidogo ila mwisho wa siku akakiri anamsupport, Jay-Z na Beyonce ni zaidi ya supporters wa kawaida kwani wao ni watu wa karibu wa Obama katika hizi harakati za kuhakikisha anarudi White House. Na slogan ya mwaka huu ni “Obama again” baada ya  ile aliyoingia nayo “Yes we can” kufanikisha mission ya ‘the black president in white house’.

No comments:

Post a Comment