Ingawa Rick Ross alifunika Fiesta Dar, Play Back zimewaacha na mshangao baadhi ya watu, wengine wasema bora wana Hip Hop wa TZ waliimba juu ya beat…


Baada ya tamasha kubwa la kiburudani Tanzania Fiesta kumalizikia Dar kwa kumdondosha Rick Rossey ambae wengi hawakumdhania kama angekuja,  sasa ni muda wa kuanza kuchambua kile ambacho kilitokea katika tamasha hili.
 Idadi kubwa ya waliopata nafasi ya kuona tamasha hili wameongea jinsi Rick Ross walivyofunika na kuwakonga nyoyo watu wengi waliohudhuria katika viwanja vya leaders, Rossey aliyepokelewa na mafataki wakati anapanda stejini, na kuendelea na shangwe za mashabiki hadi mwisho wa show, inaonesha ni kweli aliweza kuuteka umati na alipata feedback nzuri sana kuwa anakubalika sana Tanzania.
Lakini kama ilivyo kawaida zipo criticism toka kwa baadhi ya watu waliohudhuria tamasha hilo  ambao pia naamini wanaweza kuwa ni moja kati ya watu walioshangilia na kuimba na Rick Ross mwanzo mwisho lakini nao walikuwa na kitu moyoni mwao ambacho wameamua kukisema baada ya show. Ni kweli kwa jina tu la Rick Ross lina maana kubwa sana na inaweza kuwa ni sababu ya watu kushangilia sana, nyimbo wanazozipenda pia ni sababu nyingine huku wakimuona mtu huyo huyo wanaempenda sana akiwa stejini. Uwezo mkubwa wa kucheza na audience na kuwafanya wawe active mwanzo mwisho ni baadhi ya uwezo aliouonesha Rossey, ila kuna kimoja ambacho wengi wamekishangaa, ‘play back’ kwa msanii mkubwa kama huyu!
Wateja wa tamasha la fiesta waliohudhuria kwa wingi ili kumuona Rick Ross kutoka Miami Marekani, wengi walishangazwa zaidi na kitendo cha the Big Boss wa MMG kuimba kwa kundamizia nyimbo zake (play back) wakati wanajua ni international artist, wakati kuna baadhi ya wanahip hop wa hapa hapa Bongo kama Stamina waliweza kuimba juu ya beat chorus!
Wapo waliohoji inakuwaje wabongo wakienda huko nje ya nchi wanaambiwa waimbe live wakati hawa wakija huku wenyewe wanakandamizia?
Ni kweli kabisa vita dhidi ya play back ni vita ambayo wasanii wengi wa Hip Hop Tanzania wanaipagana ili wasound poa kwenye stage badala ya kuuza tu sura stejini wakati CD inacheza wimbo mzima kama redioni.
Lakini moja kati ya sababu zinazopelekea wasanii wengi hapa bongo kuimba juu ya nyimbo zao katika matamsha according to baadhi yao ni kutoviamini vifaa vinavyotumika katika matamasha mbalimbali hasa yanayoandaliwa na ma-promoter mikoani ambapo msanii anaenda bila kuwa na uhakika wa quality ya sound na microphone.
Wapo ambao wengi tumewashuhudia hata mikoani wanafanya live juu ya beat, ama kwa kutumia beat chorus, ama beat chorus yenye back vocal kumpa support ama hata kuwa na mtu special wa kumfanyia back vocal.
Sasa turudi kwa Rick Ross, hii si mara ya kwanza kwa Rick Ross kufanya play back, hata katika matamasha makubwa huko mtoni wenzake wanaweza kuimba juu ya beat kavu lakini yeye mara nyingi hua anaimba juu ya wimbo ila sauti yake kidogo inakuwa juu. Kwa hiyo sio kama alikuwa anadharau au anaangalia ukubwa wa show kama ambavyo wengi wamecomment kuhusu hili.
Nimesema hili kwa sababu wengi wametoa maoni kama haya kupitia facebook ambapo mmoja kati mashabiki waliohudhuria ameandika hivi katika mjadala mrefu uliokuwa ukiendelea katika page ya Rama Dee kuhusu show ya Rick Ross Fiesta 2012 :

“JAMAA[RICKROSS]MKALI TU STUDIO KURECORD ILA KWENYE STAGE HANA RADHA,INAWEZEKANA NI DHARAU AU KUMPAPATIKIA SANA KUKAMFANYA AFANYE KAWAIDA,CHA AJABU WANATAKA WAO WASANII WETU WAKIENDA KWAO WAPIGE LIVE ILA WAO WAKIJA KWETU KITU CHA PLAYBACK SIKULITEGEA KABSA,ZILE NI DHARAU COZ HUWA TUNAMUONA AKIWA KWAO HUWA ANAPIGA SHOW NZURI. ila jana kashndwa hata kupumua mbele ya mtoto wa mji kasoro" STAAMINA"dah mkali saaana.”
Ukiangalia BET Hop Hop awards ya mwaka 2011 aliingia kumpiga tafu Meek Mill kuimba I’mm a Boss ambayo kashirikishwa lakini aliimba juu ya verse zake za studio (play back), wakati katika tamasha hilo hilo DMX hakufanya play back, T.I na Young Jeezy as well, Wizz Khalifa, DMX, Big Sean ambao wote walitumia beat chorus hata Nick Minaj aliyeingia kumpa tafu Alicia Keys kwenye show ya MTV VMAs ya mwaka huu aliimba live pia, wakati Jay-Z hua hana muda na play back kama Rick Rossey. 

Muonekano wa Rossey stage tu huwa unatosha kuwapigisha watu shangwe za kutosha katika matamasha mbalimbali. Hata all I do is Win ya DJ Khaleed Rick Ross hua anaimba juu ya verse zake wakati wanaperfom wakati wenzake huwa wanapita juu ya beat wakisubiri chorus ya T-pain.
Kutokana na hayo tunaweza kusema kweli show ya Rick Ross ilikuwa kali sana, lakini kiukweli kabisa yeye ni msanii wa play back, na mfano wake wa kufanya play back sio mfano wa kuigwa na wasanii wa bongo japo kuna mengi mazuri ya kuiga kutoka kwake hasa jinsi ya kuongea na audience na mpangilio wa performance.

No comments:

Post a Comment