Jay-Z na Beyonce wameshindwa kulifanyia biashara jina la mtoto wao “Blue Ivy”, mahakama yampa mtu mwingine ruhusa ya kulitumia.



Akili ya biashara iliyondani ya familia ya mastaa hawa the Diva Beyonce na rais wa Rock Nation Jigga ndiyo inayowafanya kuwa couple inayoingiza mkwanja mrefu sana kwa sababu hawategemei tu muziki bali kila kukicha wanawaza kuongeza vitega uchumi, lakini sasa wameshindwa kulifanyia biashara jina la mtoto wao Blue Ivy.

Couple hii inayomulikwa zaidi na camera za paparazzi na media kiujumla ilipanga kulisajili jina la mtoto wao Blue Ivy liwe alama ya biashara yao ‘trade mark’ muda mfupi baada ya mtoto wao wa kike kuzaliwa January 2012.
Ripoti zinasema Jay-Z na Beyonce walikuwa na mpango wa kuanzisha clothing line ya nguo za watoto na ingepewa jina la Blue Ivy. Lakini jina hili (Blue Ivy) linatumiwa kama trade mark na kampuni nyingine ililoko Boston inaloitwa Blue Ivy Events Company.
Boston’s Fox 25 imeripoti kuwa Jay-Z na mkewe Beyonce wameshindwa kabisa kulitumia jina hilo na kampuni ya Blue Ivy Events ndiyo iliyopewa leseni ya kuendelea kulitumia jina hili.
October 16, judge alimuunga mkono mmiliki wa Blue Ivy Events, Veronica Alexandra aliyekuwa analitetea mahakamani jina hili kama trademark ya kampuni yake.
Kwa hali hiyo Veronica Alexandra anayoruhusa kisheria kufanya biashara bila kuingiliwa na mtu yeyote kwa kutumia jina Blue Ivy Events Company, hivyo Jay-Z na Beyonce wamezuiwa kisheria kutumia jina hili katika kutangaza clothing line yao kwa ajili ya nguo za watoto.

No comments:

Post a Comment