Rick Ross & Gucci Mane wamchana Young Jeezy ,wamtaka awape heshima.


Nitaurudia msemo uliozoeleka kuwa ‘adui wa adui yako ni rafiki yako kwa muda huo’ na hiki ndicho kinaonekana, kati ya vitu vinavyowaweka pamoja Gucci Man na Rosay sasa hivi ni ‘kila mmoja anabeef na Young Jeezy’.

Siku chache baada ya Gucci Mane kutoa wimbo aliupa jina la ‘Truth’ ikiwa ni diss moja kwa moja kwa Young Jeezy, sasa Rick Ross ameamua kumuongezea nguvu na kwa pamoja wametoa ngoma ya kumdiss Young Jeezy wakitaka awape heshima yao na ngoma hiyo wameibatiza jina “Respect”.
Katika track hiyo kuna mashairi ya moja kwa moja kwenda kwa Young Jeezy, ambapo Gucci alichana “Aint no way in hell I’ma let you desrepect me… Mad I’m fu**ng ur wifey” na Rick Rosay kiongozi wa May Back Music Group akaingia na verse yenye baadhi ya mistari kama “I push a button and them killers comin’/ Disrespect me, ni**as get nothing’.
Rosay na Young Jeezy wanabeef ambalo lilionekana waziwazi wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip-Hop awards 2012 ambapo walifikia hatua ya kusukumana wakiwa back stage.
Mwenyewe Young Jeezy alizungumzia beef kati yake na Gucci Man mwanzoni kabisa mwa mwezi huu na akasema “ Najisikia kama kila mtu anamjua yule kijana, hakuna anaemchukulia seriously. Ana Ice Cream Cone usoni. Wanasema narudi nyuma. Mimi naenda mbele. And it’s crazy kwa sababu watakuita kwenye wimbo wao. Na usipotokea kwenye huo wimbo wao, hicho ndicho kinachotokea.”

No comments:

Post a Comment