Mastaa wampongeza Drake kwa kuhitimu High School.


Drake

Kweli elimu haina ustaa na inaweza kuwa kweli kabisa tena 99.9% kuwa ni ufunguo wa maisha, pamoja na kuwa na jina kubwa sana katika ulimwengu wa muziki na kuingiza mkwanja mrefu sana, bado Drake hakukubali kupitwa na elimu, na kwa kukomaa na vyote hivi karibuni amehitimu high school na kuongeza CV ya taaluma.
Kikubwa zaidi ni kwamba Drake ameweka hadharani alama alizopata, ambapo amesema amepata 97% kwenye mtihani wa mwisho na 88% kwenye course. hizi ni alama nzuri, kweli Drake sio kilaza.
Baada Rapper huyo kutangaza hadharani kuwa amehitimu masomo ya high school watu mbali mbali wakiwemo mastaa wa Hip Hop na mastaa wa Hollywood wamempongeza, na wakati huo huo wapo watu wengi ambao wameshangaa kwa sababu hawakujua kama anasoma.
hongera zako Drake, na huu utakuwa mfano mzuri wa kuigwa na baadhi ya wasanii hasa wa bongo, wanaoacha shule eti kwa sababu ya muziki.

No comments:

Post a Comment