Fat Joe aeleza kile 50 Cent alichomnnong’oneza ili wamalize Beef: “50 whispered some things in my ear” aifananisha beef yao na Israel & Palestina




Siku chache baada ya 50 Cent na hasimu wake wa muda mrefu Fat Joe kutangaza rasmi kumaliza beef na kupanda stage moja wakati wa BET Hip Hop awards 2012 wakati wa tribute ya marehemu Chris Lighty ambae alikuwa ni mtu wao wa karibu sana, Fat Joe amefunguka kile ambacho mwenzake 50 Cent alimnong’oneza na jinsi ambavyo yeye mwenyewe alikipokea.
Joey Crack the Don kama anavyopenda kujiita alielezea katika interview aliyoifanya na HOT 107.9 “Siku zote Chriss Lighty alitaka mimi na 50 Cent tuwe na amani milele lakini tulikuwa wakorofi na tukawa tunampotezea.” Alisema Joe akielezea jitihada za marehemu Chris Lighty kumaliza beef lao, na akafunguka pia kile kilichotokea wakati wa BET Hip Hop awards 2012 alipokutana uso kwa uso na 50 Cent “nilienda kutoa heshima kwa the late Chris Lighty, nilijua 50 Cent atakuwa pale lakini nilisema tutafanya hivyo kwa sababu ya Chris Lighty tu, lakini tulipokuwa pale, 50 Cent alininong’oneza vitu sikioni kwangu vitu ambayo nilisikia ni maneno toka kwa gentleman, na nilipoyasikia nikahisi ni maneno sahihi.” Alisema Joe.
Aliendelea kufunguka “unajua mimi ni gentleman, sichukii watu. Mimi ni mmoja kati ya wana hip hop wenye upendo, amini usiamini. Lakini unajua nini, 50 alisema vitu ambavyo niliona ni sahihi kabisa, na baada ya hapo tukashikana mikono na hivyo ndivyo ilivyokuwa.”
Joe Crack anaonekana kufurahishwa pia na hayo maelewano kati yake na 50 Cent, na anaifananisha beef yake kama ile beef kati ya Israel na Palestina na kwamba maelewano yao ni kwa ajili ya Hip Hop na hicho ndicho marehemu Chris Lighty alitaka kitokee kati yao kwa muda mrefu.
“Ilikuwa ni watu wazima wawili kusema tu ‘huyu ndiye Chris Lighty, hii ni kwa ajili ya Hip Hop, tuendelee na maisha yetu.’ Hii beef ilikuwa kama Israel-Palestine, sitaki kuongea mambo mengine ya ajabu lakini hii (beef) ilikuwa inaelekea pabaya sana kivyovyote vile …lakini ghafla imemchukua mtu ambae mimi na 50 Cent tunampenda sana, mtu ambae alijaribu juu na chini kutuunganisha kwa miaka mingi.” Alimaliza Fat Joe.
Lakini pia kwenye wimbo wa Goodbye- Remix, Fa Joe ali- acknowledge jitihada za Lighty kumaliza beef lake na 50 Cent. Kwenye baadhi ya mistari aliimba anasikika akisema…
“I know you couldn’t stop the 50 sh*t/But I ain’t never look at you no different Chris/ You was my mentor, you started me/ That’s why you’ll forever be a part of me/ I pray to God to forgive him/and when you get the heaven tell Pun we’ll miss him.”
Juzi ilirushwa rasmi ile show nzima ya BET Hop Hop Awards 2012 ikiwaonesha wana Hip Hop kibao wakitoa heshima zao kwa kupokezana, na baada ya Missy Elliot kupanda na ngoma yake Get Ur Freak On, Fat Joe alipanda na ngoma yake ambayo 50 aliwahi kukiri kuwa alitamani ingekuwa yake “Lean Back.”

No comments:

Post a Comment