Baada ya kujitoa mwenyewe kwenye Kili Music Awards, sasa TID anataka kumaliza tofauti zake na waandaaji ili kutimiza ndoto zake.



Baada ya takriban miaka miwili kupita toka Khalid Mohamed a.k.a TID kuandika barua ya kujitoa na kutotaka kuhusishwa na Tuzo za muziki za Kili, leo hii hit maker wa ‘Zeze’ amesema anataka kumaliza tofauti zake na waandaaji wa tuzo hizo ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa msanii bora kwaajili ya nchi yake.
“I Really want to Finish My Differences with Kili Music Awardz so I can Pursue My Dream of becomin a better Artist for my Country”. Aliandika Top in Dar katika facebook page yake leo.
Ifuatoyo ndio barua aliyoiandika TID wakati anajitoa katika tuzo hizo mwaka 2010:
“Naomba radhi kwa mashabiki wangu wote kutoka pande zote za sayari hii najua mlikua mnasubiria kunipigia kura kwenye hiki kinyanganyiro cha award hizi za kilimanjaro,najua imekua uamuzi muafaka kwangu kujitoa kwene awards hizi basi naomba muelewe sababu zangu hizi za msingi:
1.Kwanza nahisi mimi kama TID na mziki ninao perfom kwa kipindi chote hiki cha miaka saba toka nimepewa tunzo hizi sina umuhimu wa kuwa shiriki sababu hata nikitengeza wimbo ambao unakubalika sana na wapenzi wa muziki huu wa kizazi kipya sipewi tuzo kwa mantiki hiyo naona sioni sababu ya kuwa kwenye tuzo hizi.
2.Pia nilidhani labda ni upungufu wa mawazo ya majaji ama waandaaji ambao imewezekana nilitofautiana nao kipindi fulani nilipokuwa nafanya nao kazi za maonesho,inauma sana unapoona wengine ambao uko nao kwenye same field wanapewa nafasi kubwa ambayo pia mimi nastahili kutokana na juhudi ambazo nafanya kwenye sanaa hii ya kizazi kipya hapa nahisi sihitajiki kwani kama wimbo wangu wa bendi ni bora wa mwaka kwanini nisiwe mwanamuziki bora wa kiume mwaka huo,pia hata video zangu huwa za viwango vya juu nazo hazipewi nafasi kwenye video bora za mwaka!
3.Kwa sababu hizi ambazo mimi naona kwangu hazinijengi sioni sababu ya kuwepo kwenye TUZO hizi tena kwani sidhani kama ni wakati wa kuwaangusha mashabiki wangu ambao natumia muda mwingi na effort binafsi bila ya mdhamini kuwaunganisha na muziki wangu basi nisameheni kama nimewakosea lakini hainisaidii chochote endeleeni na hao mnaowapa kila category i will never stop making good music for my country surely i wont,i was born to do THIS.”
Siku za karibuni TID ameonekana kutoa yale ya moyoni kuhusu watu ambao wamekuwa vikwazo katika maendeleo ya kazi zake za muziki, ikiwa ni pamoja na ile story ya kutaka kuumua Alikiba. Na mpya zaidi tuhuma za ku copy wimbo wake wa ‘Kiuno’ kutoka kwenye wimbo wa 'Shayman And Petersen - Fendela Fenduze' wa Zambia.
“Some FooLs are so Scared with my Sucess Walisema nataka kuwaua,Now nimecopy this KiuNo song wat is it do u Guys want From me bt u so Weak AllaH is Protectin Me!”  hii ni status aliyoiweka jumatatu wiki hii katika ukurasa wake wa facebook.

No comments:

Post a Comment