Niga C wa Jambo Squad aelezea sababu za kuachia wimbo wa ‘Dogo Mbumbumbu’, ndiye alimbatiza jina la Dogo Janja.


Niga C
Member wa kundi la Jambo squad lenye base yake Arusha City, Niga C amefunguka sababu zilizofanya aachie wimbo unaoitwa ‘dogo mbumbumbu’ambao ni diss direct kwa msanii aliyepata umaarufu akiwa na umri mdogo kwa jina la Dogo janja ambae sasa hivi anaitwa ‘Janjaro’ baada ya kudai umri hauruhusu tena kuitwa dogo.
Katika interview aliyofanya na Josefly mtangazaji wa radio Victoria Fm ya Musoma, Niga C alisema yeye ndiye aliyembatiza jina la Dogo janja na sasa aliamua kumbadilishia jina tena kwa sababu alibadikilika kitabia baada yakupata mafanikio.
“Unajua hata hili jina la dogo janja mimi ndiye niliyembatiza, nilimpa wimbo wangu unaoitwa sijisikii kufanya mapenzi na hapo ndipo jina la dogo janja lilipoanzia sasa dogo anajisikia kwamba akitoka akishapata mambo flaniflani, siunajua maskini akipata matako hulia mbwanta, ushansoma, dogo anazingua dharau nyingi nini na nini. Kwa mimi sio kwamba nimemponda pale nimemuelimisha tu. Mimi ndiye niliyempa jina la dogo janja nimemvua hilo jina nimempa dogo mbumbumbu, lakini haina maana kuwa namchukia kwa sababu nauhakika atakuja tu siku si nyingi si unajua yule ni mtoto tu. Kwa hiyo ile sio beef kwa sababu hata ukisikiliza mashairi nilioimba pale sio beef nimeongea ukweli, ningekuwa namchana mchano mwingine tofauti hapo ingeonekana ni beef. Lakini yule ni mdogo wangu nililalala nae kitanda kimoja, sahani moja tumekula, nimembeba mgongoni yule akiumwa mimi, kwa hiyo anapokuwa na kosa lazima niwe namwambia na lazima niwe namuadhibu na hapaswi mtu mwingine yeyote kuingilia kwenye swala hili, so sio beef na sio nimemdiss, nimemuelimisha kama mdogo wangu.”
Alipoulizwa kama alishawahi kuwasiliana na Janjaro baada ya kuachia hiyo ngoma ya ‘dogo mbumbumbu’ mkali huyo toka Jambo Squad wanaotamba na ngoma kibao ikiwemo Mamong’oo alifunguka, “siwezi kuwasiliana nae kwa sababu kilichosabisha nikaachia hiyo ngoma yake ni dharau zake yeye, kwa hiyo nimeshaanchia ngoma japo yeye alishanitumia message kibao yeye na meneja wake yule Ustadh Juma za matitisho matisho nini, lakini nauhakika kwa sababu yuko pale sasa hivi lakini akipata matatizo mi ndio mtu wa kwanza kunipigia simu na mimi ndio mtu ambae namsaidia siku zote yani, ushansoma, kwa hiyo mimi sioni hatari, sioni hatari yani.”
Niga C alifunguka mengi ikiwa ni pamoja sababu zilizopelekea Jambo squared kutokuwa na wa muziki na kwamba siku zote wao meneja wao ni Mungu.

No comments:

Post a Comment