Mfuasi wa Rick Ross asimulia ile fujo kati yake na wafuasi wa 50 Cent,ni kama movie, asema ingefanyika kwao Miami ‘asingesimama mtu’.



Gunplay ambae ni Member wa Mayback Music Group (MMG) ya Rick Ross the Big boss amekiri kuwa kulitokea fujo kati yake na wafuasi wa 50 Cent siku ile ya kutape tukio la BET Hip Hop award kule Atlanta.
Gunplay alifunguka na kutatua utata uliokuwa umejitokeza pale ambapo tarifa za mashuhuda wa tukio hilo lililotokea katika eneo la parking ya ukumbi ambao tukio la kutape BET Hip Hop awards lilikuwa linafanyike, walitofautiana katika maelezo waliyoyatoa, wengine walisema baada ya purukushani hizo walishuhudia Gunplay akipigwa pingu na polisi wa Atlanta, na wengine wakisema sio kweli coz jamaa hakukamatwa, lakini pia hata taarifa ya msemaji wa kitengo cha polisi alisema hakuna aliyekamatwa na hakuna aliyepata serious injuries.

Sasa Gunplay mwenyewe alitoa maelezo vizuri tu kuhusu kilichotokea maelezo ambayo yanatofautiana kidogo na taarifa za police za awali kuwa hakukamatwa, lakini mwenyewe anasema alifungwa pingu kabisa.
Gunplay alipiga story na Power 105.1 na akaelezea kile kilichotokea kwa kuwa yeye ndo mhusika mwenyewe.

“Awali ya yote,  sitataja jina la huyu jamaa kwa sababu sitaki kuharibu jina la mtu ambalo tayari limesharibika, nitamtaja kwa jina la donkey kwa sababu ni punda wa siku hii. Huyu punda anatembea na punda wengine nane, nilikuwa najiandaa kwenda kuchukua usafiri wangu, ila Police walinambia siwezi kuondoka, nilipoangalia mbele nikaona yule punda yuko na punda wengine nane na hapo ilikuwa ni mimi kuruka barrier nisepe ama nisimame tu nipandishe mshipi nikomae nao…mmoja alikuwa anatembea kunifata halafu akampa ishara flani hivi moja kati ya donkey aliokuwa nao, na mmoja alilianzisha kwa hiyo tukapambana., halafu yule mlinzi aliyenizuia nisiondoke akaja akanambia ‘toka hapa’….nilikuwa mwenyewe kama nilivyozoea kuwa peke yangu.” Alifunguka Gunplay.
Lakini Gunplay aliahidi kuwa kama hii fujo ingetokea maeneo ya Miami ambapo ndipo makao makuu ya MMG ya Rossey na hometown yao basi ingekuwa noma zaidi.

‘I ended up in handcuffs’ alisema Gunplay na kuongeza kuwa “If that would have been Miami, everybody would have been laid out” aliendelea kusema Gunplay na akaongezea kua, lakini kuonesha alivyokabiliana na hawa jamaa wa G-Unit alisema kwa sauti ya juu kuwa hakuna wa kuigusa MMG, na hakuna wa kumgusa yeye coz hata usoni hana jeraha lolote, na kuonesha jinsi alivyowakabili anasema aliwarukia hao jamaa kama simba, na kuonesha kuwa hajutii kwa kile kilichotokea na kuondoa matumani ya mtu anaedhani watayamaliza kama 50 Cent na Fat Joe, Gunplay alisema ”I don’t shake hands like the other folks.”

Siku ya kurekodi BET Hip Hop awards 2012 huko Atlanta inaonekana ilikuwa na matukio ya kutoelewana ambapo pia Young Jeezy na Rick Rossey walizinguana sana hadi kusukumana wakiwa back stage, japo taarifa za waandaji zinakanusha kuwepo kwa fujo katika tukio la kurekodi BET Hip Hop awards 2012.

No comments:

Post a Comment