Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Godwin Mjema (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa Muhula mpya wa masomo ya ngazi ya shahada ya pili ya usimamizi wa Biashara za Kimataifa.
Mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa muhula mpya wa masomo chuo cha usimamizi wa fedha (IFM) Balozi wa India nchini Tanzania Debnath Shaw (wa tatu kushoto) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) Prof. Godwin Mjema (wa sita kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wahadhiri na Walimu wa Chuo hicho baada ya kuzindua muhula mpya wa masomo chuoni hapo.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Prof. Godwin Mjema amesema Wananchi watumie fursa ya kusoma kozi  ya Usimamizi wa  Biashara za Kimataifa kwa ajili ya kujipatia ajira kwa haraka.
Prof. Mjema alisema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Muhula mpya wa masomo ya ngazi ya Shahada ya Pili ya  Usimamizi wa Biashara za Kimataifa.
“Kozi imeanza mwezi huu ambapo wanafunzi 62 wameshajiunga kwa ajili ya kupata elimu itolewayo kwa nadharia na vitendo” alisema
Alisema, kozi hiyo imekuwa ni mhimili mkubwa ndani ya nchi kutokana na umuhimu wake kwani inasaidia katika kukuza uchumi wa nchi.