JOKATE AZINDUA KAMPUNI YAKE MPYA YA "KIDOTI LOVING"




Jana katika hotel ya Serena iliyopo jijini Dar es salaam kumefanyika uzinduzi rasmi wa kampuni ya KIDOTI LOVING inayomilikiwa na aliyewahi kuwa mshindi wa pili wa miss Tanzania 2006, Jokate Mwegelo.
Kampuni ya Kidoti Loving itakuwa inajihusisha na vitu mbalimbali yakiwemo mavazi, nywele za kina dada (weaving) na mambo mengine.
Tofauti na matarajio ya watu wengi, bidhaa za Kidoti zitakuwa zinapatikana kwa bei nafuu sana na katika maeneo ambayo mtanzania wa maisha ya kawaida kabisa anaweza kuzifikia kama Kariakoo ambapo mpaka sasa tayari mzigo umeshasambazwa madukani, na hivi karibuni zitaanza kwenda na mikoani pia.


Akizungumzia nywele za Kidoti Loving, Jokate alisema:

“Ni bidhaa ambazo naweza kusema  confidently zinamfaa mwanamke wa kisasa. Ni nywele safi zenye ubora wa hali ya juu, na zinapatikana kwa bei nafuu sana”.
Akiongea na Leotainment  hivi karibuni, Jokate alisema mwanzo alianza kama hobby tu kwa kuwavalisha wasanii lakini baadae akaona anaweza kuja na kitu kikubwa zaidi na ndio ulikuwa mwanzo wake wa kuanza kutayarisha uzinduzi wa kampuni ya Kidoti Loving.
Mpaka sasa Jokate ameshawavalisha mastar mbalimbali katika video zao na maonesho yao wakiwemo Diamond Platnumz, Ommy Dimpoz na C-sir Madini katika video yake mpya ya Pain Killer.
Haya ni mafanikio makubwa sana kwa Jokate ambaye kwa sasa pia ni mtangazaji wa channel O.

No comments:

Post a Comment