Chris Brown amtukana fan aliyetaka autograph; ni baada ya kumpa mfano wa Rihanna, na kumuita ‘a wife beater’.



Kwa kawaida shabiki ndiye mtu anaefanya muimbaji yeyote awe staa kwa kumuongezea idadi ya mashabiki, lakini mambo hubadilika pale mmoja anapovuka mstari wa kuheshimiana.
Hii imemkuta shabiki mkubwa wa Chris Brown aliyekuwa na shauku ya kupata sahihi ya Muimbaji huyo kwenye CD cover yake lakini alijikuta anaambulia matusi baada ya yeye mwenyewe kuvuka mstari wa respect.
Shabiki huyo anaitwa Lucas Peter alisema kuwa walikuwa wanaangalia movie kwenye ukumbi wa Cinema wa Angeles’ Arclight  huko Hollywood na baada ya movie kuisha alimuona Chris Breezy anatoka ndipo alipoamua kumkimbilia ili asaini CD cover yake.
Shabiki huyo aliiambia Radar Online, “Bodyguard wa Chris B alinizuia na akanambia Chris asingeweza kusaini, mi nikamwambia mbona Rihanna huwa anasaini kila wakati. Hapo ndipo Chris aliposimama na akanipayukia ‘f***ot’.
Inaonekana mfano wa Rihanna kwake Chris ndio ulimkera zaidi, na hapo shabiki nae baada ya kutukanwa matusi akakasirika. Lucas aliendelea, “nilimuona Chris anaingia kwenye elevator na nikamuita ‘mpiga mwanamke’ na nikamuuliza kama atampiga Rihanna tena,” Lucas alifunguka bila kuyumbisha maneno, “Chris akasema, ‘I beat P***y’ halafu bodyguard wake akajaribu kunitishia kwa kusema, ‘na napiga wanaume pia.” Lucas alifunguka, baada ya hapo Chris akaendelea na safari yake.
Hapa unaweza kuona ni jinsi gani shabiki alionekana kukerwa na tusi alilopewa na Chris Breezy ambae inaonekana pia alikerwa na maneno ya kejeli ya shabiki huyo ambae hakupenda kukosa sahihi ya Chris. Inabidi kuwe na mutual respect kati ya shabiki na staa ili kuepuka haya.

No comments:

Post a Comment