Madonna azomewa Kwa kuwahamasisha mashabiki kumpigia Kura Obama, wengine wasusia tamasha lake.


mwimbaji mkongwe Madonna anazidi kuweka nguvu zake kumsapoti Barack Obama kwa kutumia japo dakika tatu katika tour yake ya MDNA kwa kuwa anaamini huwa anaongea na wapiga kura japo hayuko katika jukwaa la siasa. Weekend hii amekutana na changamoto baada ya kuzomewa na baadhi ya mashabiki waliokuwa katika show yake huko New Orleans alipowashawishi kumpigia kura Barack Obama.

Wakati watu wamenogewa na show, Madonna alistop kidogo na kuuliza, “nani ambae amejiandikisha kupiga kura?” Ikawa kama amepata ngazi ya kuendelea, “sijali nani mtakaempigia kura as long as mtampigia kura Obama.” Hapo baadhi ya mashabiki wakaanza kumzomea na wengine kuondoka na kuisusia concert yake.

Madonna alionekana kutokujali akaendelea, “seriously, sijali nani mtakaempigia kura…usiichukulie poa hii haki ya msingi. Nenda kapige kura.”

Inaonekana kabisa Madonna yuko serious na kumpigia kampeni Obama kila anapoona watu anaoamini ni wapiga kura kwa sababuu hii haikuwa mara ya kwanza kuwahamasisha watu waliohudhuria tamasha lake, labda nao wamechoshwa na maneno yake ya siasa.

Mwezi ulioopita alipokuwa Washington DC alitumia muda wake kuwazungumzia viongozi wa zamani kama Abraham Lincoln na Martin Luther King, Jr., akisema, “they killed him, as they do. … Ni ajabu kufikiria kuwa tuna rais ambae ni African-American ndani ya White House. Hao binadamu wema hawakufa for nothing.”

Ni kama muendelezo hivi kwa sababu majuzi kati Watu wengi ‘walimkritisaizi’ Madonna kwa kumuita Obama Muislam mweusi ndani ya White house alipokuwa katika tamasha lake kama kawaida. Lakini yeye mwenyewe alivunja ukimya na kuelezea, “nilikuwa Ironic nilipokuwa jukwaani. Kweli najua kabisa kuwa Obama sio muislam japo najua watu wengi hapa nchini wanaamini ni muislam. Na vipi kama angekuwa muislam? Point yangu ni kwamba mtu mzuri ni mzuri  tu haijalishi anaabudu nini. Sijali Obama ni dini gani- na wala mtu yeyote wa Marekani hatakiwi kujali kuhusu hili.

Presha ya kumrudisha raisi Barack Obama white house ama kumtupa kule na kumuweka Mitt Romney inazidi kupanda ikizingatiwa kuwa mwezi ujao ndio itafahamika, wanamuziki nao wanatumia kila gap wanalopata kusema kitu kumsapoti wanaemsapoti japo ndo hivo ukichanganya topic za burudani na siasa mara kwa mara ndio yanatokea haya yanamkuta Madonna.

No comments:

Post a Comment