Lil Wayne alazwa hospitalini mara mbili ndani ya saa 24, wengine wasema sababu ni ‘drug overdose’.



Rapper mkali toka YMCMB Lil Wayne ameripotiwa kulazwa hospitalini mara mbili ndani ya saa 24 kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa ni ‘seizure’, iliyompata kwa mara ya pili akiwa ndani ya private jet akitokea Texas kwenda LAX...
Mtandao wa TMZ uliambiwa na mtu wa karibu wa Weezy kuwa ndege hiyo ilikatiza safari yake na kuelekea Louisiana baada ya hali ya mkali huyo wa michano kubadilika ambapo alipelekwa hospitalini haraka kwa matibabu.
Hata hivyo taarifa za awali toka hospitalini hapo zilionesha kuwa Lil Wayne anaendelea vizuri na muda wowote angeweza kutolewa hospitalini hapo.
Tofauti na ugonjwa ambao watu walikuwa wanajua ndio unaomsumbua Weezy, Management yake ilitoa tamko kuhusu kile kinachomsibu rapper huyo baada ya taarifa za ku-seize hapo jana kwa mara ya kwanza.
“Lil Wayne aliweza kutolewa hospitalini baada ya matibabu kwa ajili ya maumivu makali ya kichwa na vilevile upungufu wa maji. Yuko nyumbani  amepumzika chini ya uangalizi wa daktari na atarudi kazini hivi karibuni. Ana-appreciate fans wake kwa sapoti yao na anawapenda.” Hilo ndilo tamko la management yake.
Ripoti zinazohusu hali ya Weezy kulazwa kwa mara ya pili hospitalini kwa ugonjwa wa ‘seizure’zilisambaa katika mitandao mbalimbali na watu wakatoa maoni tofauti tofauti kuhusu hili kwa sababu ugonjwa huu unaconnection kubwa sana na matumizi ya madawa ya kulevya.
Wengine waliuliza ‘could it have been a drug overdose??” lakini taarifa za kitaani tu zinasema alikuwa anakunywa sana siku hiyo na kuwa wanaunganisha ugonjwa huo na matumizi ya vilevi na madawa ya kulevya.
Mshindi huyo wa tuzo za Grammy aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo kama taarifa za management yake zilivyosema.
Matumizi ya madawa ya kulevya yamekuwa yakiwatesa sana mastaa nchini Marekani, hali hii ndiyo  inawafanya watu waunganishe hali ya afya ya Lil F.Baby na kutumia madawa ya kulevya kupita kiasi ‘drug over dose’.

No comments:

Post a Comment