Alicia Keys anunua jumba la kifahari la Eddie Murphy.


Lililokuwa jumba la Eddie Murphy ambalo sasa linamilikiwa na Alicia Keys

The R&B queen Alicia Keys anazidi kuthibitisha kuwa she is a girl on fire baada ya kulinunua jumba la kifahari la muigizaji maarufu duniani Eddie Murphy, jumba ambalo lilikuwa sokoni tangu mwaka 2004.
Kwa mujibu wa New York Daily News mwanadada huyo mkali wa kucheza na piano ndiye aliyenunua jumba hilo ambalo ni multi-million dollar Eglewood. Ripoti hiyo inaonesha kuwa mnunuzi ni Ms. Keys na haikumtaja Swizz Beat sehemu yoyote hivyo inaonesha kabisa kuwa Keys ameweza kwa nguvu zake mwenyewe bila kuwezeshwa.
Jumba hilo liko karibu na New Jersey, ambapo palikua maskani ya wakali kama P. Diddy na mwimbaji Wilson Pickett. Jumba hilo ambalo lilikuwa sokoni tangu mwaka 2004 lina vyumba vikubwa 32, vikiwemo vyumba nane vya kulala, sehemu za kuchezea racquetball na tennis, studio ya kurekodia muziki, elevator mbili, pool ya ndani, mabafu 10 full, na manne kama half-bath.
Eddie Murphy alitangaza kuuza jumba lake kwa mara ya kwanza mwaka 2004 kwa $30 million, na kuanza kushusha bei hiyo mara nyingi na mwaka 2010 akatangaza bei ya $ 12.75 million hiyo ni baada ya soko la nyumba za kifahari kushuka sana kuanzia mwaka 2008 kulipotokea anguko la kiuchumi marekani.
Ripoti za kuaminika zinasema jumba hilo lilitangazwa kuingia sokoni tena mwaka huu kwa mpunga kiasi cha $ 14.9 ambazo inawezekana kabisa kuwa ndizo pesa alizolipa Alicia Keys kumiliki mjengo huo wa maana.
Itakuwa kama Alicia anajiandaa kuwa na familia kubwa zaidi akiwa na mmewe Swizz Beats coz hiyo idadi ya vyumba vya kulala, ni crib ya maana sana hasa kifamilia. Hongera zake!

No comments:

Post a Comment