Ujumbe wa Ice-T kwenda kwa Obama: “No Weed Before the Next Debate Homie”


Ice-T

Rapper mkongwe Ice-T ameandika ujumbe kupitia twitter kwenda kwa Obama ambae ni mgombea wa kiti cha urais wa Marekani, ujumbe huu umekuja siku chache baada ya mdahalo kati ya Barack Obama na mpinzani wake Mitt Romney ambapo katika mdahalo huo baadhi ya watu walisema Romney alimshinda Obama, japo wengine walisema katika swala la afya Obama alifunika.
Kwa kutumia maneno machache tu kupitia tweet yake ya tarehe 05 october aliandika ‘message to the president: No Weed before the Next Debate Homie.”
Ujumbe huu uliwashangaza wengi na wengine kumjibu kuwa huo ujumbe haukuwa na ladha nzuri kwenda kwa rais wa U.S.A, tweet moja ya kumjibu Ice-T ilikuwa hii "@TarreyTorae:IceT Your Message 2 Our President is Distasteful!Thank God UR not in charge of anything that effects real life!
Hata hivyo wengi walichukulia kama Ice-T alikuwa anatania na kucomment kuwa kuna watu wengine hawatajua kama anatania. Lakini Ice-T alionekana kutojali kabisa hayo na akajibu kwa maneno yenye ukakasi.
Hata hivyo rapper mwenzake mkongwe Rah Digga pia alikiri kwamba Barack Obama hakufanya poa kwenye mdahalo huo wa kwanza.
Kufuatia maoni haya kutoka kwa watu mbalimbali kuwa Obama alifanya mdahalo chini ya kiwango ikiwa ni mdahalo wake wa kwanza, ametetewa na maoni ya watu wengine waliosema Obama ameamua kuanza hivyo ili asije akampa point Romney kwenye midahalo miwili iliyobaki, ameanza chini ili aje amkamue kwenye hiyo midahalo miwili iliyobaki.
Hivi karibuni pia kuna ujumbe uliandikwa kwa mkono ambao ulikuwa una maneno ya kushangaza na ukasambaa katika mtandao na ikasemekana kuwa uliandikwa na Snoop Lion/Doggy. Ambapo sasa inasemekana pia kuwa haukuandikwa na Snoop Lion kwa mkono wake kama habari zilivyosambaa bali uliandikwa na mtu mwingine tu. Ujumbe huo unaonesha sababu za Snoop kutomchagua Romney na sababu za kumchagua Obama, na kutaja moja kati ya sababu za kumchagua Obama ni kwa sababu mkewe Michelle ana makalio makubwa! Na Romney anaonekana kama anasema N**ga muda wote! Na mengine mengi ya aajabu ajabu.
Duuh, hivi ni baadhi ya vituko vya uchaguzi lakini sasa hapa wanaoongea ni celebs tofauti na watu wa kawaida kama ambavyo imezoeleka katika chaguzi mbalimbali hata huku Afrika, watu wa kawaida ndio huwa na utani juu ya wagombea japo pia wanaweza wasifikie kiwango hiki alichofikia ICE-T na ujumbe wake kwa Obama, na zile sababu zilizosemekana kuwa ni za Snoop Lion.

No comments:

Post a Comment