Game amlaumu Jay- Z, asema amechangia Obama Kuperform chini ya kiwango kwenye mdahalo wa kwanza: “He was probably listening to Jay-Z”.


Game

The West Coast rapper Game anazidi kuelekeza bunduki yake yenye risasi za diss kwa Jigga na sasa amekuja kivingine akimtuhumu kwa kusababisha Obama aperfom chini ya kiwango katika mdahalo uliopita.
Alipoulizwa mtazamo wake kwa performance ya Obama katika mdahalo  kwake ilikuwa ni kama alipewa gap la kumsema Jigga, Game aliunganisha tukio la mdahalo wa Obama na Romney uliofanyika mapema mwezi huu na ushiriki wa Jay-Z katika kampeni za Obama.
Alifunguka kwa kujiachia, “Nimeona mdahalo: maneno hayakuwekwa poa saana, baadhi ya mada zilikuwa covered kwa usahihi.” Baada ya hayo mawazo ya jumla, akafunguka zaidi “lakini alikuwa Obama. Inawezekana alimsikiliza Jay-Z kabla ya kuingia pale he was a little bit in the zone and couldn’t get it together. Lakini nampenda Obama ameshapata kura yangu.”
Baada ya hayo aliamua kuweka msisitizo alipokuwa anafanya mahojiano na CBS Local “ngoja nikwambie kitu, Obama angeweza kuja na akasema A-B-C zake katika hiyo debate na bado angepata kura yangu. Nampenda Obama, ametulia na ana Swag na huyo ndiye rais wangu. Mitt Romney ni wa Republican. Na siungani na chochote wanachokisimamia. Sio kama na diss imani ya mtu mwingine yeyote na anachokipigia kura, lakini mimi nampenda Obama. And he can’t do no wrong.” alimaliza Game.
Jay-Z ambae ni mtu wa karibu sana wa Obama kati ya wanamuziki wa Marekani, hivi karibuni alihost tamasha la kumchangia Obama katika kampeni zake na akatokea kwenye tangazo la kusapoti kampeni za Obama.
Jay- Z yuko mstari wa mbele katika kuhakikisha kuwa Barack Obama anarudi White house na hata katika message ya matumaini aliyoiachia Obama masaa kadhaa yaliyopita Jigga anaonekana kuifanyia kazi na kuakisi kile alichosema Mr. president.
Obama amewapa nguvu wapiga kura kwa kujiweka katika nafasi ya mpiga kura kisha akasema, “na mtaanza kuona nguvu ya kura zetu. Wakati rais anaingia ofisini mwanzoni, kile alichokipresent kwa taifa ilikuwa ni matumaini. Unajua, matumaini ya watu wote nchini ambao wangetazama na kujiona katika mambo yanayowezekana…sasa watu wanatumia haki yao, na mtaanza kuona nguvu ya kura zetu. . He made it mean something for the first time for a lot of people."
Mchakato wa kampeni unaendelea U.S.A lakini inaonekana wanamuziki wengi wanamsapoti Obama hata kama wao wanabeef kati yao lakini inapofikia hatua ya kumpigia kura Obama wanakuwa na maneno tofauti lakini yanamaana moja tu “Obama again”.

No comments:

Post a Comment