Hatimaye Justine Timberlake na Jessica Biel wafunga ndoa.


Wanandoa Timberlake & Jessica Biel

Safari ya mapenzi kati ya mkali wa R&B Justine Timberlake na muigizaji nyota Jessica Biel waliyoianza mwaka 2007 sasa imefika pazuri baada ya wawili hao kufunga ndoa na kuhalalisha mahusiano yao kama mke na mme.
Ndoa hiyo imefugwa Borgo Egnazia Resort nchini Italy katika jiji la Fasano. Mastaa hao waliwekeana ahadi za kuishi pamoja katika kila hali na kushuhudiwa na familia zao pamoja na marafiki.
Wanandoa hao wapya walionekana kuifurahia sana siku hii ya ndoa yao na kwa pamoja walisikika wakiwaambiwa watu “It’s great to be Married.”
Timbaland producer na mwanamuziki ambae ni swaiba wa Timberlake na mtu wanaeshirikiana katika muziki ni moja kati ya marafiki wa karibu waliokuwepo ukumbini.
Hakuna siku nzuri kama hii hasa kufunga ndoa na mtu ambae ulimpenda kwa siku nyingi na kuwa na ndoto ya kufunga nae ndoa siku moja na sasa ndoto hiyo imekuwa kweli, na hii ndiyo sababu ilimfanya Timbalake na mkewe Jessica kusema kwa pamoja “It’s great to be married.”

No comments:

Post a Comment