Redsan alikataa deal ya ‘jarida la fitness’ ya kupiga picha za utupu.


Redsan

Msanii wa nchini Kenya Swabri Mohammed maarufu kama Redsan amesema alikataa deal la kupiga picha za utupu kwa sababu hiyo sio tabia yake.
Katika interview aliyofanya na mtangazaji wa radio moja nchini Kenya aitwae Adelle ambae alikuwa anamuuliza kuhusu maisha yake, mtangazaji huyo alimuuliza Redsan kama alishawahi kupiga picha akiwa naked, na jibu la Redsan liliambatana na taarifa ambayo iliwashtua mashabiki wengi.
“Nakutaka” hit maker alisema hajawahi kupiga picha akiwa mtupu na hatafanya hivyo, kaisha akaongeza kuwa “actually hivi karibuni jarida la Fitness walipropose nipige picha nikiwa bila nguo, lakini nikawaambia hiyo sio style yangu.”
Watu maarufu wengi hasa waimbaji na wasanii wa kuigiza wamekuwa wakipiga picha zinazoonesha wakiwa nusu uchi ama hata wako naked, kutokana na kuwa siku za karibuni Kenya kumekuwepo na baadhi ya majarida yanayotoa mpunga mrefu kwa ajili ya matangazo ya picha za aina hiyo. Tunaweza kusema kwa kulingana na maadili ya kiafrika basi Redsan ni mfano wa kuigwa.
Mwanzoni mwa mwaka huu media zilimuandama sana Redsan baada ya kufungwa minyororo ya mapenzi na msichana aliyemaliza chuo Kikuu cha Nairobi Viverz a.k.a Lilo ambae alituhumiwa kumpiga limbwata , ‘juju’ ama Kamote kama inavyojulikana huko Kenya ili amuibe kutoka kwa girlfriend wake aliyejulikana kwa jina la Delilah.
Rumors zilizozagaa kwenye mitaa ya Nairobi zilisema mwanadada Lilo alizuga anaujauzito ili kumkoleza zaidi Redsan, na Redsan akachukua jukumu lote na inasemekana walifunga ndoa ya kwa usiri  maeneo ya Pangani.

No comments:

Post a Comment