Huu ni msala wa Trey Songs ambao umekuja kurepotiwa miezi minne baada ya kutokea.



Hii ilitokea kwenye utambulisho wa “Chapter V” albam ya sasa ya Trey Songs kwenye kitongoji cha Queens, New York Aug 21 mwaka huu, ambapo mtu mzima Trey Songs alikamatwa baada ya kumjeruhi binti mmoja kwenye mchezo unaopendwa sana na wanamuziki huko nchini marekani , wao wanauita ‘Make It Rain’..(kumwaga hela).

Ilikuwa ni mishale ya saa 10;00-10;15 alfajiri nje ya club palipokuwa panaendelea mchezo huo,  ambapo Trey alikuwa anafanya mchezo huo na katika hela alizokuwa anazirusha ,pia zilikuwepo coinz ambapo coin moja kwa bahati mbaya iliruka na kumjeruhi binti mmoja kwenye jicho lake la kushoto.
Kwa mujibu wa mtandao TMZ ishu hiyo ilimsababishia maumivu makali sana binti alitakiwa kufidiwa, na  mwezi mmoja baadae Trey Songs alikamatwa kwa kosa hilo. Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa mahakamani mwezi Feb mwakani.

No comments:

Post a Comment