Karrueche Tran awashambulia Chris Brown & Rihanna kwenye Twitter, kisa walilala pamoja usiku wa Christmas; “Wishing death upon someone is some weak s**t.”


Karruache Tran
Kati ya picha zilizo make headline sana za celebs wakisherehekea sikukuu ya Christmas, picha za Rihanna na Chris Brown zilisambaa sana na kuwa gumzo. Chris Brown ambae anamahusiano yenye drama na warembo wawili Karruache Tran na Rihanna anaendelea kuwaumiza vichwa.

Siku ya Christmas Chris Brown aliienda kuangalia game la Lakers na Rihanna, na kwa mujibu wa watu wa karibu sana wa Karruache Tran ni kwamba Chris Brown alikuwa ameshamwambia kuwa atatoka na Rihanna siku hiyo ya Christmas tena wiki moja kabla.

Hii ilionekana kumuumiza mrembo huyo lakini alivumilia tu kwa sababu alikuwa anachat na Chris Brown wakati wanaangalia mpira wa kikapu na Rihanna huko Los Angeles. Lakini hasira zilimzidia baada ya habari kuwekwa wazi kuwa Chris na Rihanna walilala pamoja usiku huo wa Christmas, na December 27, aliweka wazi hisia zake kwenye mtandao wa kijamii wa twitter kwa tweet yake ambayo ilikuwa imewekwa kimafumbo lakini inaonekana kabisa kuwa ilielekezwa kwa Chris Brown na Rihanna. 

Tweet yake ilisomeka, “Wishing death upon someone is some weak s**t.” Hii inaonesha hisia kali alizonazo Karruache ambapo inawezekana kabisa kuwa hakua na nia ya moja kwa moja ya kumuombea mtu kifa kama inavyoonekana, kwa sababu ni kitendo cha kinyonge na cha kipuuzi, lakini inaonesha jinsi gani alichukizwa na kitendo cha wawili hao kujiachia hadharani na kumdhalilisha yeye kiivo.

Hii ni kama inazunguka hivi ama tuseme ingekuwa enzi zile tungeita ‘kutesa kwa zamu’ kwa sababu hivi karibuni Karrueche alipokuwa na Chris Brown huko Paris, Rihanna alionekana kuumia sana na kumshambulia Chris kwenye Twitter.

No comments:

Post a Comment