Chris Brown na Rihanna wavurugana tena, Rihanna aandika Tweets za matusi, kisa Chris kujiachia na Karrueche Tran Ufaransa.


Karruache  (akiwa na Chris Brown mjini Paris

Inawezekana kabisa kuwa Rihanna na Chris Brown walikuwa wamekaa kwenye mstari mzuri wa mapenzi kwa kipindi hiki, lakini weekend hii imevuruga mpangilio wa mstari huo na kuwarudisha nyuma kwenye mvurugano.
Ripoti zinasema Rihanna amechukizwa sana na kitendo cha Breezy kuspend muda wake siku ya ijumaa na ex-girlfriend wake mwanamitindo Karruache Tran nchini Ufaransa weekend wakati yeye akiwa mapumzikoni peke yake.

Chanzo kimoja kililiambia gazeti la The Sun, “haimuingii Rihanna akilini kwamba Chris hawezi kubadilika, amempa nafasi nyingi sana tangu ampige mwaka 2009 na bado Chris B anaendelea kumuumiza kwa ku-party na wasichana. Kumruhusu Karruache akutane nae ni kunvuruga Rihanna na vilevile itawakera fans wake ambao wameshajua kwamba walikuwa wamesharudiana (Chris&Rihanna).”
Baada ya rumours za mwanzo kabisa kuzagaa kwenye mitandao mbalimbali na picha za Chris akiwa na Karruache T. Huko Ufaransa, Rihanna alitweet kwa hasira, “Goodbye muthaf**ker,” na tweet nyingine ilisomeka, “You give, you get, then you give it the f**k back.” Hata hivyo tweet hizi zilifutwa muda mfupi baadae.
Ijumaa Chris Brown alionekana Paris akiwa na Karruache Tran wakati huo Rihanna akiwa mapumzikoni pande za St. Tropez, na kabla ya mtafaruku huo Chris alikuwa amepanga kupumzika kidogo na kama ingewezekana angeenda kumtembelea RiRi.

No comments:

Post a Comment