Beyonce ajipanga kuuanza mwaka mpya na kitu kipya, ni kabla ya ‘Super Bowl’



Habari njema kwa fans wa Beyonce Knowles ambao wamekuwa na kiu kali wakitaka kusikia kitu kipya kutoka kwa mwimbaji huyo, ni kwamba Beyonce anatarajia kuachia ngoma mpya kabla ya tamasha la Super Bowl linalotarajiwa kufanyika February 3 mwakani.
Kwa mujibu wa The-Dream, ambae ni mtu anaeshirikiana nae sana, Beyonce atapanda kwenye jukwaa hiyo February 3 akiwa na ngoma mpya ambayo ataizindua rasmi huko new Orleans kabla hajaanza kupiga show yake kama ilivyokuwa imepangwa.

The Dream alifunguka katika interview aliyofanya na Billbord, “Definitely. Mambo yake yanaendelea. Amechukua kipindi cha summer kuanza kurecord, na sasa yupo katika nafasi ambayo yuko tayari kuanza kufichua mipango yake.”
Taarifa za kina kuhusu album mpya ya tano ya the R&B Diva Beyonce zilitolewa na Terius Nash a.k.a The Dream, na alisema katika ujio wa album hiyo na yeye amehusika katika kila hatua ya uandaaji.
The-Dream alimsaidia Beyonce kuandika nyimbo tano zilizoachiwa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment