Alicia Keys ashitakiwa kwa kuiba mistari ya mashairi ya hit song yake “Girl on Fire”.



R&B diva Alicia Keys amekumbwa na msala wa kesi inayohusiana na kuvunja sheria ya haki miliki, yaani copyright infringement kwa kunakili bila ruhusa ya mmiliki baadhi ya mistari inayosikika kwenye wimbo wake akiwa na Nicki Minaj ‘Girl on Fire’.
Keys anashtakiwa na mwandishi wa nyimbo anaeitwa Earl Shuman ambae anadai kuwa Alicia Keys aliiba mistari miwili kwenye wimbo unaoitwa “Lonely Boy” ambao aliandika akishirikiana na mwanamuziki Leon Carr na kurediwa na Eddie Holman kwa jina la “Hey There Lonely Girl” mwaka 1970 na ikashika nafasi ya pili kwenye Billboard chats enzi hizo.

Kwa mujibu wa blog ya blogger maarufu Friedman, Alicia Keys alitumia sekunde mbili tu za kwenye wimbo halisi aliokopi lakini ndizo zilizomsaidia kurekodi wimbo wake mzima wa ‘Girl on Fire.’
Mwandishi huyo mkongwe katika sanaa ya uandishi wa nyimbo ambao kwa wenzetu walioendelea wanauheshimu sana ametoa ripoti kupitia blog ya Friedman (show bizz 411) kuwa ameshafungua kesi mahakani akimshtaki Alicia Keys, kampuni ya Sony Music waandishi Salaam Remi na Billy Kravan. Katika mashtaka hayo Shuman ameeleza kuwa mshitakiwa(Alicia Keys) amevunja sheria kwa kuingilia haki miliki yake kwa hiyo anahitaji fidia ya kazi yake, ikiwa ni pamoja na faida iliyopatikana kwenye wimbo huo “Girl on Fire.”
Wakati mrembo huyo anahitajika kujibu mashtaka kwa pilato wa huko Obama land, yeye anaendeleza mashambulizi ya kuumaliza mwaka na vitu vikali na ameachia video yake mpya ya wimbo unaoitwa “Brand New Me” ambayo iko kwenye album yake ya “Girl on Fire”.

No comments:

Post a Comment