PSY wa ‘gangnam style’ aomba radhi kwa kuwatukana wamarekani jukwaani ‘Kill Those F***ing Yankees’.



Mwanamuziki toka Korea anayetamba na track yake ya Gangnam style ambayo pia ndiyo video ambayo iliangaliwa na watu wengi zaidi kwenye youtube mwaka huu, ameomba radhi kwa rap yake aliyofanya ikiwa inawatukana wamerekani mwaka 2004.
Wakati anaendelea kupata heshima kubwa sana katika ulimwengu kwa ngoma yake, media za Marekani ziliiachia hewani rap yake hiyo aliyoifanya mwaka 2004, na muda mfupi baada ya habari hiyo kuzidi kumake headline PSY alijitokeza na kuomba radhi mapema kwa wote ambao aliwakosea kupitia rap hiyo. Alisisitiza, “I will forever be sorry for rapping the provocative anti-American lyrics at his concert eight years ago.”

Aliendelea kufunguka, “kama navyojivunia kuwa Mkorea ambae nilisomea Marekani na niliishi huko katika sehemu muhimu ya maisha yangu, naelewa kujitoa kwa watumishi wa Marekani na wanawake kumefanya kulinda uhuru na democrasia katika taifa na duniani.”
Varangati hili liliibuka baada ya media za marekani kurudisha nyuma kumbukumbu za watu hadi mwaka 2004 ambapo Marekani ilipigana vita na Iraq, na wakati huo PSY alikuwa bado hajafanikiwa sana kimuziki lakini alipopanda jukwaani alirap, “Kill those f***ing Yankees who have been torturing Iraqi captives, Kill those f***ing Younkees who ordered them to torture/Kill their daughters, mothers, daughters-in-law and fathers/Kill them all slowly and painfully.”
PSY alijitetea akasema kuwa aliandika mashairi hayo akiwa katika mtafuruku mkubwa wakati wasichana wawili wa shule wa Korea na ilikuwa ni wakati ule.
“Wimbo huo niliimba miaka nane iliyopita ulikuwa ni sehemu ya hisia zangu kali kwa vita ya Iraq na mauaji ya wasichana wawili wa shule raia wa Korea na ilikuwa ni ujumuisho wa upingaji vita kwa wakati ule.”
Hata hivyo mzee wa Gangnam Style anatarajia kupiga show kubwa huko Washington katika tamasha la Christmas litakalofanyika December 21 na kuhudhuriwa na rais Barack Obama na familia yake.
Muwakilishi wa White House amethibitisha kuwa Obama na familia yake watahudhuria na wanatarajia kumuona PSY wa Gangnam Style akifanya vitu vyake jukwaani.

No comments:

Post a Comment