Baada ya tweet za mtoto wa Eminem akimvaa kwa matusi Tailor Swift, Meneja wa Rapper huyo aja na ripoti kamili.


'Hailie' mtoto wa Eminem

Meneja wa Eminem Paul Rosenberg amekanusha tuhuma kuwa binti wa Eminem Hailie Mathers alimvaa kwa matusi mwandada Taylor Swift. Meneja huyo amesema Tweet iliyosemekana kuwa ni ya jumanne, December 4, iliyoaminika kuwa imeandikwa na binti huyo sio ya kweli (ni fake tweet).
Kwa mujibu wa meneja huyo binti wa Eminem hana hata account ya twitter. Katika ripoti hiyo aliwaomba radhi fans wa Eminem na kusistiza kuwa Hailie Mathers hajawahi kujiunga na mtandao wa Twitter kwa hiyo haiwezekani ikawa katweet kumdiss Taylor Swift.

Mwanzoni ilionekana kuwa kuna mtu ambae alitumia jina la Hailie ambalo ni jina la mtoto wa kike wa mkali wa michano the Slim Shade Eminem, na kutweet, “If @tailorswift 13 is really dating the love of my life @harry styles I will not be happy!.”
Mtu huyo alionesha hisia zake kuwa hakupenda kabisa uhusiano wa kimapenzi uliochipukia kati ya member wa kundi la One Direction Harry Styles.
Mtu huyo aliendelea kutweet kumponda Tailor Swift, “Dear@taylorswif 13, please stop whoring around with every guy you see. We all know you’re only doing it so you can make another album." The fake Hailie added, "I am never, ever, everrrrr, listening to your music againnnn, @taylorswift13. LIKE EVER.”

No comments:

Post a Comment