Meneja wa Nicki Minaj aziponda tuzo za Grammy kwa kutomchagua Nicki Minaj, aziita ‘Bulls***’


Nicki Minaj

Scooter Braun meneja wa Bieber sio meneja pekee aliyeziponda nomination za tuzo za grammy ambazo hazikumtaja msanii wake kushindania hata kipengele kimoja mwaka 2013.
Cortez Bryant ambae ni meneja wa mastaa wa Young Money Lil Wayne, Drake na Nicki Minaj, nae ameziponda nomination za tuzo hizo kwa kuwa hazikumtaja msanii wake hata katika kipengele kimoja.

Meneja huyo alitweet, “Congrats to @LilTunechi and@Drake and@Hit Boy on their Grammy Noms butt....,” tweet hiyo iliyoanza kwa hongera ilimaliza tofauti kwa kuponda utaratibu wa tuzo hizo, “They was on some bulls*** for not nominating @NICKIMINAJ.”
Drake Drizzy alishare na boss wake Weezy walikuwa nominated kwa pamoja kwa kolabo lao “HYFR” NA “ The Motto”, na Drake yeye binafsi amekuwa nominated tena katika kipengele cha Best Rap Album. ‘The Harajuku Barbie’ Nicki Minaj ambae alikuwa nominated mara tatu katika tuzo hizo mwaka jana na hakupata nafasi ya kuchukua hata tuzo moja, mwaka huu hakupata nafasi hata moja ya kuwa katika kipengele chochote pamoja na kwamba ameachia album yake mpya hivi karibuni “Pink Friday: Roman Reloaded.”
Meneja wa Bieber pia hivi karibuni aliponda nomination za tuzo hizo za grammy kwa sababu hazikulitaja jina la Justin Bieber katika kipengele chochote kile ingawa anaonekana ametoa album kali, yuko katika tour yake inayoonesha kufanikiwa zaidi ‘Believe’, lakini pia kuonekana kapendwa sana na watu na kuzibeba tuzo nyingine.
Meneja huyo wa Biebs alitweet, "The hardest thing to do is transition, keep the train moving. the kid delivered. Huge succesful album, sold out tour, and won people over."
Katika tuzo hizo jina kama Lady Gaga pia hakutajwa na watu wengi waliotarajia PSY mzee wa ‘Gangnam Style’ kuingia katika nomination ya tuzo hizo, lakini wamekuwa surprised baada mwanamuziki huyo kutoka Korea kutoonekana hata kwenye kipengele kimoja.

No comments:

Post a Comment