Meek Mill Aiita Ngoma Mpya Ya Cassidy “Condom Style” kuwa Ngoma Mbovu Kuliko Zote Kwenye Historia Ya Rap.



Baada ya kupigana madongo ya chini kwa chini kupitiwa Twitter, Cassidy ilisemekana alitoa  ‘diss track’ na baadae kukanusha kwa kusema Meek Mill bado hastahili ‘a diss track’. Inavyoonekana beef kati ya Cassidy na Meek Mill linazidi kukuwa kadri siku zinavyozidi kwenda.
W’end iliyopita Cassidy kaachia ngoma mpya inaitwa “Condom Style” akiiremix ngoma ya “Gangnam Style” ya Mkorea PSY.
Baada ya ngoma hiyo kutoka Meek Mill ametumia mtandao wa kijamii wa ku-share picha wa Instagram kui’diss ngoma hiyo ya mtu mzima Cassidy. Rapper huyo aliye chini la Maybach Music Lebel ameandika…”Condom Style ni wimbo mbovu kuliko nyimbo zote katika historia ya rap…huu utani huu”…halafu akawataka fans wai’google ngoma hiyo ili waisikilize na wao pia.
Comment hiyo ya Meek Mill ni kama fans wengi wameikubali coz mara tu baada ya kuwekwa katika mtandao huo…imepata ‘likes’ zaidi ya 15,700…ndani ya miezi hii miwili mitatu…Meek Mill ameonekana kuwa interested sana na ‘rap battle’ na Cassidy…rapper ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu sasa…lets wait n see nini kitatokea.

No comments:

Post a Comment