Lady Jay dee kutoa zawadi kwa wataokaobahatisha jina la kipindi chake kipya cha TV, na kituo cha TV kitakachorusha kipindi hicho.



Umeshawahi ku imajin binti machozi Lady Jaydee on TV akiendesha kipindi chake mwenyewe cha TV?
Baada ya kuweka wazi project yake mpya inayotegemewa kuanza hivi karibuni kuwa ni kipindi kipya cha TV, sasa lady Jay dee ameamua kutoa zawadi kwa watu watano watakaotoa jibu sahihi la swali alilouliza kupitia facebook page yake kuhusiana na project hiyo, na kwamba washindi hao watashiriki katika hafla ya ufunguzi wa  kipindi hicho mwezi huu October 2012..
Jide aliandika kwenye ukurasa wake wa facebook status inayosomeka "Habarini za Leo, Nimerudi tena. Kutoa jibu la Project yangu mpya... NI KIPINDI CHA TV, ila nahitaji washindi zadi, Unaweza kubahatisha ni Kituo gani cha TV kitakachorusha kipindi hicho na Kipindi kitaitwaje????? washindi 5 watashirikishwa" katika hafla ya ufunguzi wa kipindi hicho October 2012... Kazi ni kwenu
Status hii inayotoa jibu, inaonesha kuwa huenda watu walishindwa kubahatisha kile alichosema mwezi September kuwa angetoa zawadi kwa wale watakaobahatisha ni project gani kubwa ambayo binti commando anatarajia kuja nayo katikati ya mwezi huu wa October.
September 23 Jide alipost kwenye facebook status hii "Naomba niwarushe roho kidogo kabla sijawaelezea picha halisi, Project yangu kubwa itaanza kuonekana katikati ya mwezi October 2012. Kuna mtu atakaeweza kubahatisha ni Project gani?? Washindi wa 3 watakaopatia Watapata CD ALBUM YA.5, Complimentaries za kuingia MACHOZI BAND miezi 3. Na Lunch au Dinner pamoja na mimi Siku ya Utambulisho wa Project Hiyo, Pamoja na mualiko maalum wa kuhudhuria EVENT ya hiyo PROJECT mpya. Majina ya Washindi yatapostiwa www.ladyjaydee.blogspot.com wiki moja kabla ya Project hiyo kutangazwa.".
Kama kujua project ingeweza kuwa ngumu, naamini kabisa kutaja kituo cha TV inaweza kuwa rahisi kubahatisha kwa sababu vituo vya TV ni vichache hapa bongo, kama atatumia local channels . Haya kazi kwetu kama alivyosema JIDE.

No comments:

Post a Comment