Hiki ndicho T.I anadhani kilikuwa chanzo cha ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.



Rapper T.I ambae pia ni mshindi wa tuzo za Grammy amechangia mawazo yake kwa kile kilichotokea wiki hii ambapo Rick Ross the Big Boss alizinguana vibaya na Young Jeezy hadi kufikia hatua ya kusukumana walipokuwa back stage wakati wa kurekodi matukio ya BET Hip Hop Awards 2012.

katika interview moja T.I alitaja ‘majivuno na umimi’ kuwa mara nyingi ni chanzo cha celebs  kugombana, japo alionesha kuwa ni mtazamo wake na anavyodhani ila hakujua lolote kuhusu huo ugomvi kati ya Rick Ross na Young Jeezy.
“Hata sikujua kuhusu huo ugomvi.”alisema T.I kwenye hiyo interview na akaongeza kuwa “wanaume katika sehemu yoyote, huwa tuna umimi na majivuno kwa kiasi kikubwa sana. Sijui huu ugomvi personally lakini mara nyingi ugomvi ninaousikia hua unatokana na majivuno na umimi. Lakini siwezi kuzungumzia hili kwa kila ugomvi, na sijui mengi kuhusu huu ugomvi.” Alimasema hit maker wa Leave my Life.
Lakini huu ndio mtazamo wake T.I, na kweli hata hapa bongo hii inaweza kuwa sababu mojawapo ya beef za hapa na pale za mastaa ambazo mara nyingi huwa hazina sababu za msingi kueleweka directly. 
Wikendi hii kulizuka ugomvi mara mbili wakati wa kutape matukio ya BET Hip Hop Awards 2012 kule Atlanta, kwa ndani maeneo ya back stage ilikuwa ni mtafaruku mkubwa kati ya Rick Ross na Young Jeezy ambapo camera zilinasa tukio hilo na kuonesha walinzi wakingilia kati na kuwapeleka sehemu tofauti tofauti ili wasiendelee na ugomvi huku wakitoleana makavu na inasemekana kuna baadhi ya vitu viliharibika maeneo ya back stage , na dakika chache baadae katika maeneo ya parking ya ukumbi huo kulikuwa na varangati kubwa kati Gunplay ambae ni mfuasi wa Rosay the Big Boss na wafuasi wa 50 Cent.

No comments:

Post a Comment