Sababu za Nick Minaj kutishia kumpiga Mariah Carey hizi hapa;kujisifia sana, Nick Minaj adai Carey alimuita ‘ A B*tch’ mara nyingi.



Siku mbili zilizopita habari inayohusu the first lady wa Young money kumbwatukia na kumtishia kumpa kichapo jaji mwenzake wa American Idol Mariah Carey zilisambaa katika mitandao na magazeti.
Lakini kwa haraka haraka lazima watu wengi tulijiuliza kuwa ilikuaje hadi Nick Minaj akafikia hatua ya kufungua mdomo wake na kutoa ya moyoni ghafla akiwa na jazba kiasi hicho!! Japo media zilirahisisha kwa kusema ilikuwa ni kwa sababu ya kutofautiana mara kwa mara katika kutoa maamuzi kwa washiriki wa American Idol.
Mtu wa karibu sana wa rapper huyo wa kike alisema Mariah Carey ndiye mchokozi na alichokifanya Nick Minaj ni kurudisha mashambulizi tu kwa mwanadada huyo.
“Mariah Carey alimuita Nick Minaj Malaya (b*tch) tena mara nyingi sana, kwa hiyo yeye ndiye alisababisha yote hayo yatokee” alisema mtu huyo wa karibu wa Nick Minaj. Aliendelea kuwa Nick Minaj hashawishi kirahisi kubadili mawazo kwa kile anachokiona kwa mshiriki katika mashindano hayo na kwamba Mariah Carey alikuwa anam-criticize Nick kwa hasira.
Lakini pia ripoti hizo zinasema Nick Minaj hakuweza kuendelea kumsikiliza Mariah Carey kwa sababu Carey anapoteza muda mwingi sana kujisifu yeye mwenyewe badala ya kufocus katika kuwapima na kuwachambua washiriki wa shindano hilo.
Mtu mwingine ambae anafatilia sana mashindano ya American Idol aliuambia mtandao wa TMZ kuwa “Marih Carey analeta story binafsi kuhusu mauzo ya record zake, watu aliofanya nao kazi, ziara ngapi ameshapiga na tuzo ngapi za Grammy ameshauza…sasa Nick hayo yameshamchosha.”
Lakini bado hatujasikia kwa upande wa the R&B diva Mariah Carey nae naamini atakuwa na la kusema na kuitetea nafsi yake dhidi ya kile kilichofanyika na kinachosemwa juu yake.
Hivi karibuni Nick Minaj alimbwatukia Mariah Carey na kumtishia kumpa kichapo wakati wanaendelea na kazi ya kuwajaji washiriki wa American Idol katika maeneo ya Charlotte, North Carolina, wakati wamekaa kwenye meza moja na katikati yao alikaa jaji mwenzao Keith Urban, na jaji mwingine aitwae Randy Jackson akiwa amekaa upande wa mwisho karibu na Mariah Carey.

No comments:

Post a Comment