Madonna achojoa nguo akiimba wimbo kwa ajili ya msichana wa Pakistani aliyepigwa risasi kichwani, ‘Why!’


Madonna

The queen of pop Madonna ameamua kumsupport msichana Malala “Yousafzai” (14) aliyepigwa risasi kichwani na askari wa Taliban, ila support ya Madonna imekuwa ya aina yake ambapo aliimba wimbo wa Human nature kama dedication kwa msichana huyo huku akivua taratibu  nguo zake moja baada ya nyingine.
Madonna alikuwa katika concert ya tour yake ya MDNA Los Angeles, na Wakati anaendelea na tamasha lake ghafla alisimama na akasema “wataliban walimsimamisha na kumpiga risasi. Do you know the sickness and absurdity of this?” baada ya kuwaweka sawa audience akaongea kwa sauti ya juu “Support education!” kisha ukafata wimbo wa ‘Human by nature’ huku akivua nguo zake taratibu moja baada ya nyingine.
Kufuatia kitendo hicho alichofanya Madonna kinacholeta mkanganyiko hasa ukifikiria connection kati ya kuvua nguo na kusupport harakati za msichana aliyepigwa risasi na askari wa Taliban, watu wengi wamem-criticize sana Mwanamuziki huyo mkongwe. Mtu mmoja alitweet “Not the right way to pay Homage to Brave Malala. It’s a way to earn cheap self popularity,” na mwingine akatweet “Does Madonna understand how stupid and offensive cavorting in her bra on behalf of Malala Yousafzai is? The Taliban will love it.”
Malala Yousafzai, ni msichana mwenye umri wa miaka 14 ambae alipigwa risasi akiwa katika gari la shule kwa sababu aliandika kwenye blog kuhusu umuhimu wa elimu kwake, akipigania haki ya kupata elimu kwa watoto wa kike.

No comments:

Post a Comment