Karruache Tran achukizwa na Video aliyoitoa Chris Brown akisema anawapenda wote yeye Na Rihanna, asema maneno matatu tu…!


Karruache
Karruache Tran msichana mrembo ambae kwa sasa anaonekana yuko katika kipindi kigumu akiwa na stress za kuachwa na mtu aliyempenda kwa moyo wake wote kisha akapeperuka na kurudi kwa girlfriend wake wa zamani Rihanna.
Pamoja na maumivu yote hayo ya kuachwa lakini inaonekana kitu kingine kilichomuumiza zaidi ni pale Chris Breezy alipoweka hadharani feeling zake tena akiwa amelewa na kuieleza dunia nzima kupitia video clip. Alichofanya Chris B kwa Karruache ni  kama kumwagia spirit jeraha la moyo wake ambao umeumizwa sana.
Karruache kwa hasira alikuwa na maneno matatu tu ya kumwambia Chris kwa uchungu “shut your mouth.” na hakuwa na la ziada nadhani kwa sababu ya maumivu ya moyo, si unajua tena kuachwa ni shughuli pevu.
Watu wa karibu wa Karruache waliuambia mtandao wa TMZ kuwa mrembo huyo alichukizwa sana kwa sababu Chris Brown alianika matatizo yao binafsi kwenye mitandao kwa kutumia video yake ya kipuuzi akiwa amelewa na kukiri kuwa anawapenda wote Rihanna na Karruache. Watu hao wa karibu wa Karruache waliongeza kuwa kama Chris B alidhani hiyo video ingesaidia kulainisha ukweli kuwa ameamua kumuacha K.T basi ‘he dead wrong’.
Taarifa kutoka kwa best friends wa Karruache zinasema mrembo huyo angependa Chris B azitunze hizo feeling zake moyoni mwake na sio kuzianika kwenye mitandao na video hiyo inamuumiza zaidi na kum-disappoint mrembo huyo.
Hivi karibuni Chris aliweka Video kwenye mtandao inayomuonesha yeye akiwa kalewa amekaa chini na anaelezea feeling zake kuwa anawapenda wote Rihanna na Karruache Tran, na hii ni baada ya muda mchache kutangaza kumuacha rasmi Karruache eti ili asiharibu urafiki wake na Rihanna na asiendelee kumuumiza mwanadada huyo kumbe alikuwa na lake la ziada moyoni.
Katika video hiyo Chris anaonekana kama na yeye ana stress na ameamua kunywa pombe ili kuzipunguza coz yuko kwenye dilemma. Lakini video hiyo inaonekana iko planned na imetengenezwa kwa kiwango kizuri ikiwa na title “The real Chris Brown”.

No comments:

Post a Comment