Huyu ndio Nick Minaj bila make up, angalia Trailer ya kwanza ya reality series yake.


Nick Minaj akiwa bila make-up

Rapper wa kike toka Young Money ameamua kuonesha trailer ya reality series yake ambayo itaonekana siku 21 ikiwa na sehemu tatu na ameipa jina la ‘Nick Minaj: My Truth’.
First lady wa Young Money ameamua kutoa trailer ya series hiyo ikiwa inaonesha nyuma ya pazia ya maandalizi ya concert yake, maandalizi ya album yake pamoja na kuwa jaji wa ‘American Idol’. Watu wataanza kuwatch series hiyo kuanzia November 4 na itarushwa kupitia channel ya E!
Nicki Minaj ameahidi kuonesha maisha yake ya kweli kabisa hata kabla ya kupigwa make up ili kuonekana mbele ya video.

Minaj bila make-up
“mtaniona bila make up, sura yenye jasho ndani ya studio, unajua, vile vitu vya kawaida.” Hayo ndiyo ambayo anaahidi Nicki yataonekana kwenye series yake. Akafunguka zaidi kuwatease fans wake, “mtaona mazoezi yangu kwa ajili ya tour. Watu huwa wanaona upande wa tour yangu nikiwa tayari nimeandaliwa na kila kitu kikiwa kimeshawekwa sawa.”
“mtaona behind the scene ya vitu vingi...mtaona nasema navyofeel kuhusu watu wanaonifanyia mahojiano,  na sehemu nzuri na maalum ninayoipenda ni kwamaba inaonesha watu ambao wananizunguka, watu ninaowapenda, watu ambao inabidi niwe nao kila siku na itatuonesha hivi vitu vipya ambavyo vinatokea kwangu.” Alimaliza Nicki Minaj kuhusu ‘her truth.’

No comments:

Post a Comment