ULEVI NOMA: Wameishi miaka 20 ndani ya ndoa halali bila kujua, walifunga ndoa wakiwa wamelewa.


Mchekeshaji Janeane Grofalo

Katika hali ya kawaida watu hufunga ndoa wakiwa wamekubaliana kwa asilimia 100 kuishi kama mke na mme kwenye shida na raha, afya na ugonjwa. Lakini utimamu wa akili kwa asilimia 100 unahitajika katika hili, na tilalila kupita kiwango flani hupunguza utimamu wa akili kwa asilimia kadhaa.
Janeane Garofalo ambae ni mchekeshaji maarufu huko Marekani, alienda New York kuhudhuria tamasha la wachekeshaji ‘The Ben Stiller Show”, na huko alifunguka kuhusu ndoa yake na ex-husband wake ambae ni producer wa ‘Big Bang Theory TV Show’ Robert Cohen kuwa walifunga ndoa miaka 20 iliyopita, lakini hakuna hata mmoja kati yao alikuwa anafahamu kuwa ilikuwa ni ndoa halali kwa sababu wote walikuwa tungi a.k.a tilalila wakati wa tukio hilo tena kanisani.
Garofalo alisema yeye na mmewe walianza kudate tangu miaka ya 90 na usiku mmoja wakiwa wamelewa walipitia kanisani huko Las Vegas na kufunga pingu za maisha, na wote hawakuwahi kufikiria kuwa ile ndoa ilikuwa ni halali hadi siku ambayo mwanasheria wa mmewe huyo wa zamani Cohen alipogundua wakati Cohen wanajipanga kufunga ndoa nyingine ya halali na mtu mwingine baada ya kuachana na mchekeshaji huyo ambapo kisheria iliwabidi watafute talaka ya ile ndoa yao ya kilevi kwanza.
“Sisi tulidhani ulitakiwa kwenda mahakamani kusaini makaratasi, so who knew?” Galofaro alinukuliwa na New York Post.
Galofalo na Cohen walitalakiana kisheria katika eneo la TD Bank, Midtown dakika kadhaa kabla mchekeshaji huyo hajaingia kwenye tamasha hilo, “Rob na Mimi tulikuwa na ndoa, kiukweli,na tumeimaliza kwa talaka dakika 30 kabla sijaingia hapa,” alifunguka Galofalo, na kumaliza kwa mshangao, “we were married for 20 years until this evening!”
kwa kawaida talaka hua inafaida na hasara zake, ikiwa ni pamoja na mtoa talaka kufidia baadhi ya gharama ama kugawa mali walizopata wakiwa wawili, japo walikuwa hawajui kama ni wanandoa wawili hao sasa watapata haki zao kwa kufaidika na mkwanja alioingiza kila mmoja wakiwa kama mke na mme katika kushirikiana.

No comments:

Post a Comment