Jim Jones amtaja Cam’ ron kama the best rapper….na kusema Juelz Santana angekuwa na mafanikio zaidi ya Jay z.


Jim Jones

Japokuwa albam inayosubiriwa kwa muda mrefu ya washkaji walioungana na kujiita The Diplomats imebaki fununu tu ndani ya miaka kadha, hiyo haina maana kuwa washkaji hawako vizuri baina yao.
kwenye interview na jarida la SOHH, mmoja kati ya rappers wanaounda kundi hilo..Jim Jones amepata nafasi ya kuwazungumzia washkaji zake alionao ndani ya The Diplomats ambao ni Cam’ron na Juelz Santana.
Katika interview hiyo Jim Jones amezungumzia vitu vingi lakini hapa nadondoka na viwili tu kati ya hivyo…la kwanza ni pale alipolist down top five favorite rappers kwake yeye ambapo aliwataja Fabolous, Lil Wayne na Rick Ross.
Hakuishia hapo…akamalizia kwa kumtaja mshkaji wake Cam’rom kama his best rapper on earth….na kusema Juelz Santana angekuwa msanii mkubwa hata zaidi ya Jay Z.
“Namzungumzia Juelz Santana…siku zote namwambia angeweza kuwa na mafanikio hata zaidi ya Jay Z…huyu mtoto ana kipaji cha pekee…hebu sikiliza kila anachokifanya na muziki wake unasema nini..na Cam’ron…nadhani Cam ni best rapper….basi…ninamfahamu Cam na nimekuwa nae…nimeona, nimeshuhudia na nimetazama yote kuhusu muziki wake…kwahiyo ni ngumu sana kushinda hili…ni ukweli na halisi”…amemaliza Jim Jones.

No comments:

Post a Comment