Nicki Minaj ambwela na “Pink Friday: Roman Reloaded – The Re Up” Wiki yake ya kwanza kitaa..



Wakati jana tulifunguka na story kuhusu Rihanna kudondosha machozi ya furaha  baada ya “Unappologetic” kutangazwa kushika nafasi ya kwanza kunako the no one albam chat in America..Billboard Top 200 Albams Chat kwa kuuza nakala 238,000 katika wiki yake ya kwanza tu kitaani, leo tunakuja na mauzo ya albam iliyotoka siku moja Nov 19 na albam hiyo ya Rihanna na kila mjuzi wa burudani akiamini kuwa ni albam itakayo’battle na “Unappologetic” ya Rihanna.
Hii si nyingine bali ni albam ya Harajuk Barbie…1st lady toka YMCMB…Nicki Minaj..”Pink Friday: Roman Reloaded-The Re Up”. Cha kushangaza ni kuwa japo Nicki alitegemewa kuweka upinzani mkubwa kwa Rihanna lakini cha ajabu ni kwamba ishu imekuwa tofauti kabisa.
Hata hivyo Nicki Minaj mwenye alipata nafasi ya kuzungumzia hilo alipofanya interview na New York City Radio siku chache baada ya albam kuingia mtaani na kusema hategemei kuuza sana wiki yake ya kwanza kwa sababu eti baadhi ya maarufu ya mauzo ya albam Marekani yamekataa kuhusika kuuza mzigo huo…ni ya kweli hayo?? au alishaona dalili sio nzuri??
Wakati “Pink Friday: Roman Reloaded” iliyotoka April 12’ 2012 iliuza nakala 253,000 wiki yake ya kwanza….“Pink Friday: Roman Reloaded-The Re Up” imeuza nakala 36,000 tu wiki yake ya kwanza. Hata hivyo imeruka kutoka nafasi ya 95 mpaka nafasi ya 26 kunako Billboard Top 200 Albam Chat….katika HipHop na R&B mzigo huu umeshika nafasi ya nne wiki hii baada ya “Unappologetic” (Rihanna), “Woman To Woman” (Keisha Cole) na “good kid, m.A.A.d city” (Kendrick Lamar)…Lets wait n see.

No comments:

Post a Comment