Ni ngumu kuamini, Tasnia ya burudani imempoteza Sharo Millionea , R.I.P


Haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kuziamini habari zilizoanza kuenea usiku wa jana kupitia mitandao ya kijamii facebook, twitter na hata bbm kuwa, mchekeshaji maarufu nchini Tanzania aliefahamika kwa jina la Sharo Millionea ameaga dunia baada ya kupata ajali ya gari huko muheza Tanga.

Huu ni uthibitisho wa kifo chake kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Tanga kama alivyofanya mahojiano na millardayo.com

“kwenye majira ya saa mbili usiku barabara ya Segera Muheza mtu mmoja alietambulika kwa jina la Hussein Ramadhani au Sharo Milionea akiwa anaendesha gari namba T478 BVR Toyota Harrier akitokea Dar es salaam kwenda Muheza alipofika eneo la Maguzonizonga wilayani Muheza hilo gari lake liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali Teule ya wilaya ya Muheza”
 
Ni msiba mkubwa kwa watanzania wote hasa wapenda burudani kutokana na usheshi aliokuwa nao na kufanikiwa kuwa na mashabiki wengi. Tulikupenda zaidi Sharo Millionea lakini ni kazi ya Mungu.

No comments:

Post a Comment