Project mpya ya Solo Thang: Siasa Ujinga Maradhi Na Umasikini (S.U.M.U)



Mteule Solo Thang anaendelea kufanya kazi ya muziki kwa nguvu, baada ya kutoka na album ya  'I am A Travellah'  sasa ameamua kuandaa project nyingine aliyoipa jina la ‘S.U.MU’ (Siasa Ujinga Maradhi na Umasikini).
Wiki iliyopita Solo thang kupitia blog yake aliandika hivi:

“ Juzi kati nilitimba studio za Roof records ndani ya mitaa ya Dublin Ireland kwa mara ya kwanza tangu nilipotoa Album ya I AM TRAVELLAH vol 1,,chini oya producer TONY,,nashkuru siku ilikua nzuri na kilichopikwa  kimepewa jina la SUMU ambapo kirefu chake ni SIASA UJINGA MARADHI na UMASIKINI!
S.U.M.U ndio itakua project mpya yangu kwa lugha ya kiswahili,,itakua na ngoma zaidi ya  14,,project hiyo inatarajiwa kuwa tayari mwakani kipindi cha summer!”

Labda tungejiuliza vipi Solo anakuja na album ama ni mixtape tu, yeye mwenyewe alifunguka,“Hii sio tu Album,hizi ndio zitakua HARAKATI zangu kijamii, zenye nia ya kuondoa SUMU hii hatari!”

No comments:

Post a Comment