Moto wa Nick Minaj kwenye ‘my truth’ waanza na Mariah Carey “nadhani kipidi hiki amekutana na size yake”


Reality Series yenye matukio kibao nyuma ya lens yanayomhusu rapper wa kike wa Young Money Nick Minaj ilianza kurushwa rasmi November 4 na kwa kuanza tu imeanza na moja ya vipande ambavyo wengi walikuwa wanavisubiri ambapo amemtupia words Mariah Carey ambae ni jaji mwenzake katika ‘American Idol’ na walikuwa na beef kali mwanzoni tu mwa mashindano hayo.
Katika sehemu hiyo ya kwanza ya reality show yake ‘My Truth’ amemzungumzia Mariah Carey na jinsi yeye mwenyewe alivyokuwa anadoubt kujiunga na American Idol.
“Nadhani kipindi hiki Mariah amekutana na saizi yake, na sidhani kama alitegemea kukutana na saizi yake.” Alifunguka Minaj, lakini alionesha kuwa na wasiwasi kuhusu American Idol alisema “I’m super nervous and anxious for the first day on American Idol. Bado nawaza mara ya pili kuhusu uamuzi wangu. Labda ntaendelea kuwaza mara mia kuhusu huu uamuzi kwa sababu mimi ni binadamu. Ni kazi kubwa.” Alifunguka kukweli wake rapper huyu wa kike ambae ingekuwa TZ kiarusha tungesema hua anakalisha matembo.
Hayo yote ni yale ambayo yanatokea nyuma ya pazia katika matukio tofauti tofauti yanayomhusisha Nick Minaj kama alivyowaahidi fans wake. Lakini alifunguka ukweli kuwa mwanamitindo wake alikosea kutoa maamuzi yake kwa kile alichokivaa Nick Minaj masaa machache kabla ya kuingia kwenye auditions za American Idol, na kila alichokuwa anachagua kuvaa Nick Minaj alikipa jina ‘ugly’ a.k.a kibaya.
Kipande kingine kilichoonekana kilimuonesha Nick Minaj akiwa na stress katika siku ya kwanza tu ya American Idol. Ambapo alionekana kumind kuchelewa katika siku ya kwanza tu ya mashindano hayo ya kusaka vipaji vya kuimba. “huwa siangalii vitu kichwani. Ntaviona pale nitakapoviangalia kwa macho. Ukinambia kuchagua kitu wakati niko nervious na anxious, nitapata tatizo katika kila kitu. ..This is 911. Dee-sester.” Na akasisitiza tena kuhusu uchelewaji “ ntachelewa kama lisaa lizima au hata masaa mawili? Mnajua kimaandishi hii itakuwa inakera kiasi gani? Kwamba nimechelewa katika siku ya kwanza tu.”
Hapo alikuwa anajipangapanga kwenda kuungana na majaji wenzake wa American Idol Keith Urban, Randy Jackson na mwimbaji wa kike the Diva Mariah Carey ambae walianza kuzinguana mapema wakati mashindano hayo yanaanza na Nick Minaj akafikia hatua ya kumtishia kumpiga.
Reality show ya member huyu wa Young Money “My Truth” itaendelea kwa siku 21 ikiwa na sehemu tatu ikiwa ni maandalizi ya kuikaribisha album yake mpya yenye nyimbo 27 ‘Pink Friday: Roma Reloaded-The Re-Up’ ambayo imeshatanguliziwa ngoma mpya na kali ‘Freedom’

No comments:

Post a Comment