Chris Brown avaa kigaidi kwenye party ya Rihanna, ashikilia bunduki fake mkononi.


Chris Brown (katikati) na kundi lake

‘Turn up the music’ hit maker Chris Brown aliwashangaza watu baada ya yeye na kundi lake kuingia kwenye party ya Halloween ya girlfriend wake Rihanna wakiwa wamevaa mtindo wa kitalban ama mtindo wa kigaidi.
Chris ambae alionekana akiwa ameshikilia mkononi bunduki fake na kuionesha juu, hakuwa na mengi  ya kusema lakini chini ya picha yake na kundi lake alitweet “Ain’t no body F**n’ wit my clique.”

Chris na Rihanna waki-hug
Ripoti zinasema Chris alifika saa moja kabla ya Rihanna hajafika kwenye party hiyo. 

Breezy mwenyewe hakuwa na la kuongeza zaidi ya statement aliyotweet, lakini mama yake anaeitwa Joyce Hawkins, alisema “Halloween is for fun nothing more than just fun.”

Japokuwa Chris Brown alionekana kwenye Halloween party nyingine akiwa na Karrueche lakini inaonekana kabisa kuwa yuko serious zaidi na Rihanna kwa sababu hata mama yake Chris Brown mwenyewe alialikwa kuungana nao kwenye Halloween pary ya Rihanna alionekana akifurahi sana akiwa na Rihanna (mama yake Chris).

Kwa kawaida Halloween party ni sherehe ambazo hufanyika kila mwaka hasa usiku wa October 31 ukiwa ni usiku wa kuamkia siku ya watakakatifu wote.
Ukiweka kando hayo mengine ya utani anaoufanya na mkasa wao wa mapenzi, Chris ameendelea kufanya mazuri katika jamii na hivi karibuni ameanzisha ‘Symphonic Love Foundation’ mbayo inalengo la kusapoti  program za sanaa kwa vijana na kuhamasisha huduma za kijamii, heshima na wema. 

Synmphonic Love inaimani kubwa na uwezo wa ‘sanaa na upendo katika kuibadili dunia.’

No comments:

Post a Comment