Wakati Alicia Keys amenunua jumba la kifahari, mmewe ‘Swizz Beatz’ anaandamwa na madeni ya kodi.


Swizz Beatz

Producer mkali Swizz Beatz ambae ni mme wa ‘the girl on fire’ hit maker Alicia Keys ameendelea kukumbwa na msala wa madeni ya kodi. Akiwa ndiye the latest celeb kupata msala huu producer Swizz Beatz anadaiwa na serikali ya jiji la New York $ 98,246.18 kama kodi ambayo hakuilipa mwaka 2010. Beatz pia anadaiwa kodi nyingine na serikali ya jimbo hilo kiasi cha $ 2.6 Million.
Hii sio mara ya kwanza kwa jina la producer huyu kutokea kwenye list ya majina yenye madeni ya kodi. June 2010 alikuwa anadaiwa na serikali $652,727 kama kodi ambayo hakuilipa mwaka 2008 kama income tax. Ambapo mwanasheria wake alisema wanajadiliana na serikali kuona ni jinsi gani wanaweza kunegotiate ili wamalize tatizo hilo la kodi la Beatz mwaka huo 2010.
Mwaka 2011 aliripotiwa kuwa anadaiwa zaidi ya $2 million na serikali. Lakini pia ripoti za kipindi hicho zinasema yeye na ex-wife wake Mashonda walifunguliwa kesi ya madai ya kodi New York, Georgia na Calfornia.

Ingawa anakumbwa na madeni hayo yote, Swizz Beatz ni producer anaeaminika sana kwa kazi zake, na kwa mujibu wa Forbes alishika nafasi ya 16 katika list ya top ten ya Hip Hop Cash Kings ambayo ilitoka September ikimuonesha Beatz akiwa anaingiza $ 7 million (income).

Jumba la Alicia Keys
Wakati madeni ya kodi yanamuandama Swizz Beatz, Mkewe Alicia Keys hivi karibuni alifunika zaidi na kuprove kua she iz a girl on fire baada ya kununua jumba la kifahari la muigizaji Eddie Murphy ambalo lilikuwa limewashinda matajiri wengi likiwa mnadani tangu mwaka 2004 na kukutana na kisu kikali cha mkwanja wa Alicia Keys. Hati ya jumba hilo iliandikwa jina la Alicia ikimaanisha halina uhusiano na ushiriki wa Swizz Beatz katika kulinunua.
Swizz B anajiandaa kudondosha album yake na DJ Khaled ikiwa ni album ya kwanza ya Beatz ndani ya mika 12. “It’s not all the way in stone yet because Khaled is super busy. I’m super busy. The Lox are super busy, but it’s a main goal for us to really make that happen,” Swizz aliimbia RapFix Live.

No comments:

Post a Comment