Rihanna na Chris Brown kufanya wimbo wa pamoja “Nobody’s Business”


Baada ya kuwa topic kwenye media kibao kuhusu mapenzi yao ku-break up na ku-make up sasa Breezy na RiRi wamekuja kivingine na kutoa habari njema kwa fans wao kuwa wanatarajia kuachia ngoma nyingine ya pamoja baada ya muda mrefu wa milima na mabonde ya uhusiano wao na kwamba wimbo huo utakuwa katika album ijayo ya Rihanna “Unpologetic”.
The ‘take a bow’ hit maker Rihanna ametangaza kupitia Twitter collaboration yao na Chris Brown ikiwa ni pamoja na kuachia rasmi list ya ngoma zitakazokuwa kwenye album yake hiyo ya saba “Unpologetic”.
Hii itakua ni mara ya tatu mwaka huu kwa wawili hao kufanya project ya pamoja. Mara ya kwanza ilikuwa ni mwanzoni kabisa mwaka huu “Birthday Cake”, na pia kwenye remix ya Chris Brown “Turn Up the Music”.
Hizi collaboration angalau zinatoa nafasi chanya kwa Breezy na Rihanna kwa fans wao ambao kuna wakati walikuwa wameanza kugawanyika kutokana na kuwepo mtafaruku kati yao.
Breezy yupo katikati ya muda wake wa kuwekwa katika probation ya miaka mitano baada ya kumpiga ‘the Umbrella girl Rihanna’ mwaka 2009 siku moja kabla ya usiku wa tuzo za Grammy.
Album ya “Unpologetic” inatarajiwa kuachiwa rasmi November 19 wengine waliopewa shavu ni Eminem, Mikky Ekko na Future.

No comments:

Post a Comment