Lil Wayne asema anafikiria kustaafu baada ya “The Carter V”.



Feb 19 mwaka 2013 CEO wa Cash Money Young Money Brothers (YMCMB) Lil Wayne ataachia mzigo wake mpya kama muendelezo wa mzigo wake wa mwaka 2010 “Am Not a Human Being”. Lakini kabla ya undani wa habari hizi haujagonga vyombo vingi vya habari, Lil Wayne mwenyewe amejitokeza na kusema anafikiria kustaafu muziki hivi karibuni.
Kwenye Interview yake na MTV Lil Wayne amesema ana mpango wa kustaafu muziki na hiyo itakuwa baada tu ya kuachia “The Carter V” sehemu ya tano ya muendelezo wa series yake hii.
Rapper huyo kutoka New Orleans amesema kwa muda aliokaa kwenye game hii umepelekea kuwa na passion ya kufanya mambo mengine lakini yaliyo ndani ya muziki huu huu.
“Najua wote nyie mnataka niendelee kuwepo kwa muda zaidi lakini “The Carter V” ndo albam yangu  ya mwisho. Nimekuwa niki-rap tangu nina miaka 8 na nina miaka 30 sasa…huu ni muda mrefu…na nataka nifanye vitu vingine vingi zaidi…na nnapokuwa nataka kufanya jambo huwa nakuwa na haraka sana…napenda kufanya kitu…ninatazama hicho hicho tu…na unaweza kuwa sio”..alimazila Lil Wayne.

No comments:

Post a Comment