Kim Kardashian azishangaa tetesi za kuwepo mipango ya ndoa kati yake na Kanye West.


Wakati watu wanasubiri kuona Kanye West anavuta jiko lake ili wawe na uhalali kama mke na mume, yaani K.K angechukua talaka yake rasmi toka kwa mumewe wa zamani Kris Humphries halafu ajikabidhi kisheria kwa Kanye, mrembo na mwanamitindo Kim Kardashian anaona kama ni kichekesho flani tu na anashangaa hizi rumors zinatoka wapi.
Hivi karibuni executive producer wa Kadashians Ryan  Seacrest alisema kuwa Kanye West amepropose kwa girlfriend wake Kim Kardashian.
K.K alionekana kushangaa sana tetesi hizi ambazo wengi walikuwa wanaziamini kwa kuwa aliyesema ni mtu wa karibu sana, K.K alisema, “Mi sijui Ryan amepata wapi hili.” Akaendelea kufunguka huku akicheka, ”Ryan, am so mad at you, umepata wapi haya? Unaanzisha rumors.”
Hizi rumors zilizidi kuzagaa na kuonekana kama ni ukweli hasa pale ambapo Kim alionekana akiwa kavaa gemstone ring kwenye kidole chake cha pinky wakati anarudi Marekani baada ya kutoka katika mapumziko na Kanye West.
Kinachoshangaza hakusema kitu chochote wakati huo hadi hivi karibuni wakati watu wameshaamini ndipo amekanusha tetesi hizo, “ni tetesi tu, lakini birthday yangu ilikuwa poa sana, very intimate and very special.” Alimaliza Kim Kardashian.
M-baby wa Boss wa G.O.O.D MUSIC ataendeleza shangwe za birthday yake na party kubwa ya Halloween huko Miami ambako mastaa kibao watadondoka. Mwenyewe K.K alisema, “Halloween is one my favorite holidays.”

No comments:

Post a Comment