Baada ya rappers wengi kuingia kwenye msala huu, Nas aripotiwa kuingia pia….



Awali mtu mzima Nas Escoba alishawahi kuwa na matatizo ya kukwepa kulipa kodi na alikuwa na deni la zaidi ya dola 6 milioni, now serikali ya jimbo la Georgia ina msala mwingine kwa Nas na sasa ni dola 1 milioni.
Kwa mujibu wa TMZ serikali ya jimbo la Georgia limefaili legal documents ya makusanyo ya kodi ambayo Nas hakulipa mwaka 2006, 2007, 2009 na 2010, na idara ya mapato ya jimbo hilo imeitaka Live Nation kuchukua mapato kutoka kwenye tour ya hivi karibuni ya Nas na Lauryn Hill.
Muwakilishi wa Nas amesema ishu hiyo tayari ishawekwa sawa na kesi kwenye Idara hiyo ya mapato bado iko wazi na wako katika mchakato wa kulipa madai hayo.

No comments:

Post a Comment