Janjaro amchana Niga C wa Jambo Squad baada ya kutoa ‘Dogo Mbumbumbu’, “sinaga masihara na watoto washambawashamba hawajui fadhira…”


Janjaro
Mkali wa michano toka Ngarenaro Arusha Dogo Janja ama Janjaro kama anavyopenda kuitwa sasa hivi baada ya kufikisha umri unaofaa kukanseli jina dogo, ameyatoa yake ya moyoni kama kawaida baada ya kuisikia ngoma ya Niga C inayoitwa ‘Dogo Mbumbumbu’.

Katika interview aliyofanya na Josefly mtangazaji wa Radio Victoria fm ya Musoma kwenye show ya Over Drive, Janjaro alianza kwa kukana kuwa Niga C hakuwa rafiki yake kama Niga C anavyodai, ila walikuwa wanajuana kwa ajili ya mambo ya muziki tu na kila mtu alikuwa anahustle kivyake .

“Hakuwa ni rafiki yangu lakini tulikuwa tunajuana tu katika mambo ya muziki na yeye alikuwa kundi lingine na mimi nilikuwa kundi lingine  na kila mtu alikuwa anahustle kivyake na najua unachotaka kuniuliza kwamba jamaa anajitahidi kuisafiria nyota ya mtu lakini kitu ambacho hakiwezekani, karekodi wimbo mzima ambao kanitukana mimi, lakini mimi kama mimi niliona kama ni changamoto na anazidi kunipa vina, naomba tu mzidi kumpa interview za radio azidi kuniponda, ntashukuru sana”.

Janjaro alikana sauti ambayo ukiisikia unapata jibu tu ‘ni dogo janja’ akiiponda hip hop na kuisifia bongo fleva, “hapana, sikia, huyo jamaa kuna kitu kakifanya ambapo kamchukua mtu ambae ana sauti inafanana na ya kwangu, hata hiyo nyimbo mara ya kwanza mi kuiskia ilikuwa ni kwenye kituo kikubwa cha radio Dar es salaam na sijui lolote kwa sababu huyo jamaa mi nilikuwa nawasiliana nae kuhusu maswala ya muziki, tunakaa mtaa mmoja….kwanza hatukai mtaa mmoja Ngarenaro imegawanyika sehemu nyingi, yeye anakaa…mi nakaa darajani, tofauti. Yule mtoto wa bibi mimi town hustler kitambo sana yaani, way back kinoma yaani. Lakini kaamua kusafiria nyota ya mtu haina noma Mungu ndiye anapanga bana, kama katoa wimbo wa kunitukana…afu ukiangalia eti anasema kanisaidia, yeye anafanya muziki katuni mi niko real, yeye anafanya mashairi yanatoka mifukoni, mistari gani, tangu lini mashairi yanatoka mifukoni.” 

Janjaro alifunguka mengi ya moyoni na stori za maisha yake na Niga C, jinsi alivyomsaidia Niga C alipoenda dar akalala kwa Ustadh Juma ambae anamsaidia Janjaro kimuziki.

Pamoja na michongo mingine, Josefly alitaka kujua kama umri wake wa miaka 18 aliyoifikisha mwaka huu unamsaidia vipi kusolve matatizo kiutu uzima kwa sababu ameshakosana na member wa Tip Top na sasa ni Niga C ambae ni mshikaji wake wa zamani.

Hapo mzee wa ‘kukalisha matembo’ akafunguka, “sinaga masihara na watoto washambawashamba hawana mpango ambao hawajui fadhira, ndo kuwakwepa hivyo, mtu unacheka nae vizuri halafu baadae anakuja kukusnitch!”

Mwishoni akatoa namba kwa mashabiki wake kwa ajili ya kumuuliza maswali ambayo ni namba tofauti kabisa na ile aliyokuwa anatumia muda huo, na akasema hiyo ni special kwa ajili ya mashabiki wake tu wenye maswali kwake.

Hivi karibuni Niga C wa Jambo Squad ambae pia alikuwa mshikaji wa karibu wa Dogo janja ( Janjaro)  aliachia wimbo wa unaoitwa ‘dogo mbumbumbu’ akimchana Janjaro. Lakini pia alieleza sababu za kuutoa wimbo huo.

No comments:

Post a Comment